Tanzania na Rwanda zinakamilisha mchakato wa ujenzi wa reli itakayounganisha mataifa hayo mawili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Hayo yamesemwa Jana Jumatano November 27, 2019 na Rais Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Isaka Mkoani Shinyanga.
“Nimeshazungumza na Rais Kagame (Paul wa Rwanda) kuhusu utekelezaji wa mradi huu, upembuzi yakinifu umekamilika. Kinachofanyika sasa ni kutafuta fedha,” alisema Rais Magufuli.
Reli hiyo itakayounganishwa na ile ya kati itaanzia bandari kavu ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mradi huo ambao tayari hatua ya upembuzi yakinifu umekamilika utarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari kavu ya Isaka kwenda nchi jirani.
Social Plugin