Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb) leo Jumamosi ameweka Jiwe la Msingi Jengo la Taasisi ya Umoja Wa Vikundi Majohe(UVIMA) lililopo katika kata ya Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Said Kumbilamoto kwa naiba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mwenyekiti wa UWT (W) Ilala Bi Amina Omary George.
Mhe. Mama Salma Kikwete ameahidi kuchangia Bati 100 ili kusaidia kukamilika kwa ujenzi wa Jengo hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb) akizungumza wakati wa akiweka jiwe la msingi jengo la Taasisi ya Umoja wa Vikundi Majohe (UVIMA) lililopo katika kata ya Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Social Plugin