Na.Faustine Gimu Galafoni.Dodoma
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy mwalimu amesema serikali inaendelea na mchakato wa kuboresha sera mpya ya afya ili kuimarisha huduma za afya nchini badala ya kuendelea na sera iliyopo kwasasa ambayo imepitwa na wakati.
Waziri Ummy amesema hayo jana Nov.27,2019 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la sita la afya nchini lijulikanalo “TANZANIA HEALTH SUMMIT “ambapo pamoja na mambo mengine ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwasilisha bungeni muswaada utakao lazimisha kila mtanzania kuwa na bima ya Afya.
Waziri Ummy amesema Sera ya Afya ya Mwaka 2017 imejikita zaidi katika masuala ya tiba na si kinga hivyo Sera Mpya ya mwaka 2019/2020 itajikita zaidi katika Masuala ya kinga kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Aidha ,Waziri Ummy amesema katika sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2019/2020 itaangalia mktadha wa kuwafikia wananchi huduma ya Afya yaani Afya kwa wote kwa kuangalia vigezo muhimu vya uhitaji tofauti ya na sera ya iliyopo ambapo inasema zahanati kila kijiji bila kuangalia mzigo wa Magonjwa ama geografia ya eneo husika.
Kwa upande wake Rais wa Kongamano la Afya nchini Tanzania, Dokta Omary Chillo amesema Lengo la kongamano hilo ni kujadili changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya afya na namna ya kukabiliana nazo ili kuleta ufanisi zaidi katika utendaji kazi.
Kongamano la sita la Afya Mwaka 2019 limeanza Nov.27 hadi 28,2019 huku likiandaliwa na Taasisi sita ambazo ni Wizara ya Afya Tanzania,Wizara ya Afya Upande wa Zanzibar ,Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Tume ya Huduma za kijamii ya Kikristo,Baraza la Waislam Tanzania[BAKWATA] na Tindwa Medical Services na kaulimbiu ni ufanisi na Matokeo katika utoaji wa huduma za Afya.
Mwisho.
Social Plugin