Watu 15 wamenusurika kifo baada ya breki za basi la abiria la kampuni ya Harambee kushindwa kufanya kazi na kupelekea basi hilo kupoteza uelekeo na kuyagonga magari mengine wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amesema ajali hiyo ilitokea jana jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.
"Ni kweli kuna ajali imetokea jana jioni eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi , majeruhi walikuwa 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine walipata majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wakapewa huduma ya kwanza," amesema Kamanda.
Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.
Tazama picha za CCTV.
Watu ambao idadi yao haijajulikana wamenusurika kifo baada ya breki za basi la abiria la kampuni ya Harambee kushindwa kufanya kazi na kupelekea basi hilo kupoteza uelekeo na kuyagonga magari mengine wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.Tazama picha za CCTV. pic.twitter.com/Sb3G9i1W7c— Azam TV (@azamtvtz) December 18, 2019
Social Plugin