Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Casmir Mabina amewasilisha barua makao makuu ya chama hicho ya kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi wa kanda hiyo ambayo yamemfanya aliyekuwa mgombea uenyekiti, Fredreck Sumaye atangaze kukihama chama hicho.
Mabina ameeleza uamuzi wake huo leo Jumatano Desemba 4, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Haya Mambo yametokea ndani ya eneo langu la kazi na kwa maana hiyo leo Jumatano nimewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi yangu.
"Nitabaki kuwa mwanachama mwaminifu wa chama chetu na nitakuwa tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika.” Amesema
Social Plugin