MABIBI HARUSI WASHONWA SEHEMU ZA SIRI KUWA MABIKRA

Bibi harusi na bwana harusi wakicheza densi nchini Sudan

Katika msururu wa barua kutoka Afrika, mwandishi Zeinab Mohammed Salih anaangazia swala la ukeketaji kwa mara ya pili nchini Sudan.

Baadhi ya wanawake nchini Sudan Kusini wameamua kufanyiwa ukeketaji mwezi mmoja ama miwili kabla ya harusi yao ili 'kujifanya kuwa mabikra'.

Hili linafanyika hata ijapokuwa wengi wao tayari washafanyiwa ukeketaji wakiwa wasichana - kitu ambacho hufanyika kati ya miaka 4 na 10.

Katika taifa hilo ambalo ni la Kiislamu - ukeketaji huo unahusisha kutolewa kwa sehemu za siri na unashirikisha kushonwa ili kupunguza upana wa sehemu nyeti.

Uzi uliotumiwa kushona sehemu hiyo hukatika wakati mwanamke anaposhiriki ngono.

Iwapo mwanamke anayetarajiwa kuolewa atafanyiwa ukeketaji zaidi na mkunga , maeneo zaidi ya siri yatakatwa na kuushona uke.
'Hataweza kutembea kwa siku kadhaa'

''Ilikuwa uchungu sana na nililazimika kwenda na kukaa na rafiki hadi nilipopona kwasababu sikutaka mamangu ajue'' , alisema Maha ambalo sio jina lake la kweli ili asitambulike.

Kukojoa lilikuwa swala tata na hakuweza kutembea kwa siku kdhaa.

Maha alifanyiwa upasuaji ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa harusi yake ambapo alifaa kuolewa na mtu ambaye umri wake ni mkubwa kumliko.

''Hangeweza kuniamini iwapo angegundua kwamba nilishiriki mapenzi kabla ya ndoa yetu'', alisema. ''angenizuia kwenda nje ama hata kutumia simu''.

Msichana huyo aliyefuzu na kupata shahada kutoka chuo kikuu ana umri wa miaka 20 na anatoka katika jimbo la Kaskazini mwa Sudan ambalo linapiga marufuku ukeketaji

Lakini kitendo hicho bado kinaendelea kufanyika - ikiwa asilimia 84 ya wanawake wa Sudan walio na umri wa kati ya miaka 14 hadi 49 wamefanyiwa ukeketaji kulingana na Umoja wa Mataifa.

Na ijapokuwa Maha anafanya kazi katika mji wa Khartoum ambapo tendo hilo ni haramu aliamua kwenda nyumbani ili kukeketwa na mkunga kwa njia ya siri.

Anamjua mkunga , ambaye alikubali kufanya operesheni hiyo kwa chini ya pauni 5000 za Sudan ambazo hutozwa.
'Nakata kwasababu nahitaji fedha'

Katika tamaduni nyingi ambapo ubikra kabla ya ndoa ni muhimu , wanawake hupendelea kufanyiwa upasuaji ili kuziba uke wao, ili kuweza kuficha vitendo vyovyote vya zamani vya wao kushiriki kingono.

''Upasuaji huo hufanywa na mpasuaji na haupatikani nchini Sudan na nimeambiwa kwamba kliniki moja inatoa huduma hiyo kwa wanawake walio katika ndoa pekee. Hivyo basi kushonwa ili kupunguza upana wa uke ndio chaguo bora''.Image captionKwa kawaida mfumo wa Infibulation huwa ni kushona sehemu ya uke na kuacha tundu ndogo tu

Baadhi ya wakunga pia hupendelea kukata baadhi ya sehemu nyeti wakati wa upasuaji huo.

Mkunga Dkt Sawsan alisema mwanaharakati wa kukabiliana na FGM nchini Sudan anasema kwamba mabadiliko yoyote katika uke hutambulika kama ukeketaji aidha mtu awe ameshonwa ama kutobolewa.

Hatahivyo hakuna utaratibu unaoweza kufanyika hospitalini, hata Khartoum kwa kuwa baraza la matibabu nchini Sudan haliruhusu.

Litamfuta kazi mkunga yeyote atakayepatikana akitekeleza kitendo hicho na kumpokonya vifaa vyake.

Ijapokwa katika hospitali tatu nilizotembelea , wakunga walifurahia kunipatia taratibu zinazochukuliwa. Mmoja wao hata alizungumza hadharani mbele ya wauguzi wengine na kunionyesha vyumba ambavyo uketeteji unaweza kufanywa.

"Je ungependelea kukata eneo nyeti{ clitoris?} Iwapo hutaki mimi nishike .. sitashika...lakini nitakata eneo la labia na kuzishona pamoja'', alisema.

Mkunga mwengine alisema kwamba alikua tayari kufanya ukeketaji huo lakini mara nynegine alihitajika kufanya hivyo ili kuweza kupata fedha.

Niliishona njia ya uke wa msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa amebakwa na binamu wake.

''Mamake alikuja hapa na kulia hivyobasi nilitaka kuwasaidia'', alisema.

''Nilikula kiapo cha kutowakata wanawake ama wasichana tena, lakini mimi hufanya hivyo mara moja moja kwa kuwa ninawalea wajukuu wangu, ambao mama yao alifariki na nahitaji kulipa karo zao za shule''.

Mradi wa Saleem uliozinduliwa 2008 unasaidiwa na Umoja wa mataifa kusitisha kitendo hicho cha FGM nchini Sudan.
Enzi mpya?

Itachukua muda mrefu kubadili tabia kama hizo hususan katika jamii ya kihafidhina.

Natumai kwamba mke wangu atakuwa bikra,aliniambia mwanamume mmoja ambaye hajaoa mjini Khartoum akisema kwamba atamshuku kufanya mapenzi na watu wengine nje iwapo hilo halitakuwa limetimia.Itachukua muda mrefu kubadili mtazamo kuhusuukeketaji katika jamii ya kihafidhina.

Hii ni tabia ya kawaida kote Sudan ambapo wanaume hutarajia wanawake kushonwa.

Ijapokuwa wanaharakati wa FGM wana matumaini kwamba mambo yatabadilika kutokana na hatua ya serikali mwezi uliopita kubadilisha sheria moja ya umma ambayo inadhibiti jinsi wanawake wanavyoendelea na shughuli zao za kawaida na mavazi wanayovalia mbele ya umma, ikiwemo kupiga marufuku wanawake kuvalia suruali ndefu.

Sheria hiyo ilianzishwa takriban miaka 30 ya utawala wa rais Omar al Bashir ambaye alipenduliwa akiwa rais mwaka huu kufuatia maandamano ya umma.

Chini ya sheria ya kuweka amani katika maeneo ya umma , mamlaka ilikuwa na haki ya kuamua kile ambacho wanawake wanapaswa kuvalia , wanaozungumza nao, na kazi yoyote watakayofanya- huku yeyote anayekiuka sheria hiyo akiadhibiwa kwa kuchapwa viboko ama katika visa vingine anapigwa mawe hadi kufa na hata kunyongwa.

Nahid Toubia, mwanzilishi wa An Lan - kundi la wanaharakati wa kukabiliana na ukeketaji kutoka Sudan anasema kwamba wanawake wadogo hii leo wamepiga hatua ikilinganishwa na wazazi wao.

Wanadhania kwamba wana haki ya kushiriki ngono lakini pia wanalazimika kujishona mara ya pili ama hata kuvalia Hijab kabla ya harusi yao.
CHANZO- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post