Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Infotech Investment Group ambaye aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, Ali Mufuruki (60), amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Disemba 8, 2019 akiwa Afrika Kusini akipatiwa matibabu.
Mufuruki ni kati ya matajiri wakubwa 10 wa Tanzania akiwa ni mmiliki wa Kampuni ya Infotech Investment Group Limited na maduka ya Wolworth.
Oktoba 18, 2019 Mufuruki alijiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania ili kupata muda zaidi wa kuendelea na biashara zake.
Mwenyekiti wa sasa wa Ceort, Sanjay Rughan amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kilichotokea saa tisa alfajiri katika Hospitali ya Morningside.
Social Plugin