Na Salvatory Ntandu - Kahama
Wazee 2271 katika Halamshauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamepatiwa kadi za bima ya afya iliyoboreshwa (CHF) ambazo zitawasaidia kupata matibabu bure kwa mwaka mzima na kuondokana kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba.
Wazee wasiojiweza waliosajiliwa na baraza la wazee la Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga ni 6247 na waliopatiwa kadi za CHF ni 2271.
Hayo yalibainishwa jana Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa Halmshauri ya Mji kahama, Willfred Bilago wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini kahama alisema hapo awali wazee walikuwa wanahangaika kupata matibabu kutokana na kukosa kadi za CHF iliyoboreshwa.
“Wazee tulikuwa tunaona ni bora kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba mbadala kuliko kwenda katika hospitali ambapo tulikuwa hatuthamini na wengi wetu walipoteza maisha kutokana huduma hizo zisizokuwa za kitaalamu”alisema Bilago.
Alisema kadi za CHF zimesaidia wazee wasiojiweza kupata huduma za matibabu ambapo kwa unafuu na haraka kwani katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa kahama kunadirisha la kuhudumia wazee na madaktari maalum kwa ajili wao.
“Tunawaomba wadau,wafanyabiashara,viongozi wadini kusaidia upatikanaji wa kadi za CHF kwa wazee wasiokuwa na waangalizi ili waweze kupata matibabu bure kwani suala hili tukiiachia serikali pekee kwani nasi tunawajibu wa kuwatuza wazee wetu” alisema Bilago.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Abel Shija alisema kuwapatia kadi za CHF wazee katika halmashauri hiyo ni takwa la kisheria hivyo hawana budi kulitekeleza agizo hilo.
Kwa mujibu wa sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 inazielekeza halmashauri kuhakikisha haki za wazee waliofikia miaka 60 zinalindwa pamoja na kuwapatia huduma bure za matibabu.
Social Plugin