Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Loy Mhando
Mapema mwaka huu Tanzania kupitia sekta ya viwanda ilibainisha kutenga ekari 127,859 kwa ajili ya viwanda katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Aidha jitihada hizo zimepelekea jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa hiyo chini ya uongozi wa sarikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa viongozi mbalimba akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na waziri wa viwanda Mh. Innocent Bashungwa ,serikali imejipanga kuweka mazingira sawa na mifumo ili kuboresha biashara na viwanda kwa kuweka mazingira rahisi na nafuu.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) inayosimamia urasimishaji wa biashara na majina ya kampuni imeboresha mifumo ya utendaji wake na kurahisisha ili kuwawezesha wafanyabiashara kurasimisha jina la biashara, kusajili majina ya kampuni, alama za biashara na viwanda mahali popote walipo kupitia tovuti ya wakala
Aidha Waziri Mkuu anataja Viwanda vilivyojengwa kuwa ni vya kuzalisha bidhaa za ujenzi (Saruji, Nondo, Vigae, Mabomba, Marumaru, n.k); pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo Nafaka, Matunda, Mafuta ya kupikia na bidhaa za Ngozi.
Mkakati wowote wa kukuza uchumi unawategemea sana wafanyabiashara, Tukiwa kwenye kilele cha miaka 20 tangu Wakala Wa Usajili wa Biashara na Leseni kuanzishwa ni mambo mengi tunajivunia ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa urasimu na rushwa uliokithiri uliokuwa katika taasisi hiyo.
Heko na pongezi nyingi ziende kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kwa kubuni mfumo Madhubuti wa urasimishaji kwa njia ya mtandao Online Registration System (ORS)
Tangu mfumo huo wa (ORS) kuanzishwa yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tu zaidi ya makampuni 7000 yamerasimisha Biashara na kusajili majina ya Biashara na Kampuni. katika mfumo huo hivyo kufanya shughuli za urasimishaji wa biashara na viwanda kwenda kwa haraka zaidi kupitia mfumo huo wa (ORS).
Tathmini iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu imeonyesha kwa mwezi BRELA walikuwa wakirasimisha Biashara na kusajili majina ya Biashara na Kampuni. 60 tu lakini sasa kwa mwezi wanarasimisha Biashara na kusajili majina ya makampuni 750 mpaka 800 jambo ambalo linadhihirisha na kuonyesha mafanikio makubwa kwa muda mfupi sana.
Kwa zaidi ya asilimia 50 urasimu na michakato mirefu ya kupata vibali na leseni za biashara pamoja na uwekezaji umepungua kwa kiasi kikubwa.
Kujirasimisha kwa mtandao kunamuwezesha mfanyabiashara kutambulika na hivyo kuingia kwenye mfumo wa ushindani kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.