KATIBU MKUU WA CCM AAGIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUWASHUGHULIKIA WADOKOZI NA WEZI KWENYE MIRADI


Katibu mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akiongea na wananchi wa halmashauri ya Bukoba.
Katibu mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akiongea na wananchi wa halmashauri ya Bukoba.
Katibu mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akikagua eneo la hospitali ya wilaya ya halmashauri ya Bukoba.

Na Ashura Jumapili -Malunde 1 blog Bukoba.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM )Dkt Bashiru Ally ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha wale waliofanya kazi za ufundi, vibarua, wahudumu na kazi zingine katika miradi mbalimbali ya serikali wanalipwa kwa wakati hasa kwa miradi ambayo serikali imetoa fedha hizo.

Bashiru ametoa maagizo hayo leo Desemba 27, 2019 alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya halmashauri ya Bukoba , ambapo licha ya kuridhishwa na ujenzi huo amedai amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali ya wafanyakazi kutokulipwa kwa wakati licha ya fedha zote shilingi bilioni 1.5 kufikishwa hospitalini hapo.

Dkt. Bashiru ,alisema wakuu wa mikoa na wilaya wasisite kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na warudishe fedha wasimamizi wa miradi hiyo ambao wamekula fedha na kushindwa kuwalipa wafanyakazi kwa wakati ili jasho la wananchi wanyonge lisipotee.

’’Natoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchi nzima, kuhakikisha wanalinda miradi hii dhidi ya wadokozi na wezi wa rasilimali hizi za wananchi, na wale wote waliotoa jasho lao kujenga mradi huu, yaani mafundi, vibarua, wahudumu na wafanya kazi wengine, walipwe kwa wakati na jasho la mwananchi lisipotee, kama kuna waliohusika katika kuchelewesha malipo yao, wachuliwe hatua kali za kinidhanu kwa mujibu wa sheria za nchi.” Katibu Mkuu amesisitiza.

Aidha, Bashiru alitoa wito kwa wenyeviti wote wa vijiji na mitaa nchi nzima kutoa ardhi kwa shughuli za jamii ikiwemo ujenzi wa Hospitali, Shule, Ofisi za umma, na kadhalika kama ambavyo imefanyika katika kijiji cha Kanazi kwa wananchi kujitolea eneo ambalo ujenzi wa hospitali hiyo ya halmashuri unaendele, ambapo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

“Nawashukuru sana wanakijiji cha Kanazi kwa kujitolea eneo hili kwa ujenzi wa Hospitali hii ya Halmashauri, na ninatoa rai kwa wenyeviti wote wa aserikali za mitaa na vijiji toeni ardhi kwa matumizi kama haya, na mfano huu wa kijiji cha Kanazi uigwe nchi nzima’’,alisema.

Ambapo aliongeza kuwa, utaratibu wa kugawa ardhi za vijiji ni lazima uwe shirikishi na ufanywe na mkutano Mkuu wa kijiji au mtaa na si wajumbe wa halmshauri ya kijiji pekee ili kupunguza migogoro na kuweka maamuzi kuwa ya uwazi kwa wananchi wote kama ilivyofanyika kijiji cha Kanazi.

 Dkt Bashiru alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuiamini CCM na serikali yake chini ya Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, ambapo ameweza kudhibiti nidhamu katika serikali na Chama, na mafanikio yanayopatikana sasa ya ujenzi wa Hospitali nchi nzima, vituo vya afya, zahanati, Barabara, Madaraja, Umeme, miradi ya maji n.k ni matokeo ya jitihada hizo.

Halmashauri ya wilaya ya Bukoba ni miongozni mwa halmashuri tatu za mkoa wa Kagera zilizopokea fedha za ujenzi wa hospitali za wilaya, nyingine ni karagwe na Kyerwa

Awali, Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bw. Deodatus Kinawilo akimkaribisha Katibu Mkuu, ameeleza namna serikali ya wilaya, ilivyoridhidhwa na maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo licha ya changamoto mbalimbali ikiwemo hali mvua kwa muda mrefu ujenzi uliendelea na sasa kufikia hatua ya umaliziaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post