CHADEMA WAFUNGUKA BAADA YA SUMAYE KUTANGAZA KUKIHAMA CHAMA HICHO


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa na kauli za  mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye aliyetangaza kukihama chama hicho.



Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam uliofanyika leo, Sumaye ametangaza kujitoa Chadema huku akitoa tuhuma mbalimbali kwa  mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa chama hicho hakikuwa na taarifa za mkutano huo uliofanyika leo  na kwamba wameona barua tu mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.

Mrema amesema wamezipokea taarifa za Sumaye kuondoka Chadema na kama mwanachama yoyote ameacha pengo kwenye chama hicho,  kwamba watatafuta namna ya kuziba pengo hilo.

“Hatuna taarifa za makundi kwenye chama chetu l kama anavyodai Sumaye, labda kama yeye alikuwa na kundi.  Sumaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama alikuwa na nafasi ya kutoa taarifa hiyo na kama kweli ipo ingefanyiwa kazi.


Kuhusu uchaguzi wa chama hicho unaoendelea, Mrema amesema katiba ya Chadema hairuhusu mgombea kupita bila kupingwa,  kama mgomba ni mmoja lazima apigiwe kura ya ndio au hapana.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post