Chama cha Wananchi CUF kimesema kuwa kimeazimia kurejesha ofisi zake zote zilizochukuliwa na chama cha ACT Wazalendo hususan Visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaama na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Mussa Haji Kombo, ambaye alisema kuwa ofisi hizo ni mali ya CUF hivyo ni lazima wazirejeshe.
“Kwa kuwa baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limeazimia kurejesha ofisi zake zilizoporwa na ACT kupitia kikao chake cha hivi karibuni sisi viongozi tutazirejesha na tupo tayari kwa lolote na wala hatuna hofu na vitisho vya Maalim Seif na wafuasi wake.
Katika hatua nyingine, Kombo alimtuhumu Maalim Seif kuwa ni mbaguzi na mwenye kupandikiza chuki miongoni mwa jamii ya watanzania.
Social Plugin