MKURUGENZI wa Halmashauri ya Pangani Issaya Mbenje akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa yaliyofanyika kwenye Kata ya Madanga wilayani Pangani mkoani Tanga kushoto mwenye miwani ni Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja
Kaimu mratibu wa Huduma za VVU Mkoa wa Tanga Rose Kiluvia akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho hayo
Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Upimaji magonjwa mbalimbali ukiendelea kwenye maadhimisho hayo
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje katika akiwa na awadau mbalimbali wakitoka kukagua moja ya mabanda yaliyopo kwenye viwanja ambavyo kulifanyika maadhimisho hayo
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje kulia akiteta jambo Ofisa Mradi wa Taasisi ya Mkapa Foundation Dkt Anastazia Masanja mara baada ya kukagua mabanda
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje kushoto akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wataalamu wakati alipotembelea mabanda
OFISA Mradi wa Taasisi ya Mkapa
Foundation Dkt Anastazia Masanja amesema kwamba licha ya elimu kuhusu ugonjwa
wa ukimwi kutolewa miaka mingi jamii bado jamii haijabadilika katika suala zima
la kuwanyanyapaa watu wanaishi na maambuzi wa virusi vya Ukimwi.
Dkt Anastazia aliyasema hayo katika
maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa yaliyofanyika kwenye Kata
ya Madanga wilayani Pangani mkoani Tanga ambapo alisema hali hiyo imepelekea
watu kuwa na hofu kipima afya zao kwa kuhofia kunyanyapaliwa.
Alisema changamoto ya unyanyapaaji pindi mtu anapobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi
imekuwa ni kubwa hasa katika wilaya za Handeni, Pangani na Kilindi huku
akiitaka jamii kuachana navyo.
Ofisa huyo alisema tokea wameanza programu ya upimaji
inayofahamika kama “Furaha yangu”wamefanikiwa kupima watu 45,515 katika kata 30
za wilaya hizo ambapo watu 708 walikutwa na maambukizo ya ugonjwa huo.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kaimu mratibu wa
Huduma za VVU Mkoa wa Tanga Rose Kiluvia amesema katika Mkoa wa Tanga
waliogunduliwa kuwa na VVU na Ukimwi tangu kipindi cha mwaka 2002 hadi 2019 ni
238,872 na watu 32,190 walikufa.
Naye kwa upande wake Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Issaya Mbenje, alisema ili kufikia
asilimia 95 tatu ambayo ni lengo la serikali ifikapo 2030 kuhakikisha kiwango
cha maambukizi kimepungua ifikapo mwaka huo.
Alisema tatizo la maambuzi ya VVU na Ukimwi ni kubwa na
changamoto katika ya jamii ni maendeleo kwenye mkoa wetu wa Tanga na hiyo ni
kulingana na matokeo ya utafiti wa kitaifa vya vuiashiri vya malaria na ukimwi
vya mwaka 2017/2018.
Alisema viashiria hivyo vinaonyesha kiwango cha maambukizi ya kitaifa ni asilimia
5.1 na kwa mkoa wa Tanga hali ya maambukizi
ni asilimia 5.0 maana yake kati ya watu 100 watu watano wana maambukizi ya virusi
vya ukimwi.
Taasisi hiyo ya Mkapa Foundation imeanza shughuli zake Julai
mwaka 2018 katika wilaya za Pangani, Handeni na Kilindi lengo hasa ni kutoa
elimu na kuifanya jamii kuwa na hamasa ya kuondokana na maambukizi mapya pamoja
na jamii kujijengea utaratibu wa kupima afya zao.
Mwisho
Social Plugin