Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford akitoa salamu za UNICEF wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtathimini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Mr. Hong Vu akiendesha chemsha bongo wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakifurahia jambo wakati wa chemsha bongo kwenye kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu, Mwenyekiti wa TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete pamoja na Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (katikati) akitoa maelezo mafupi kuhusu ESRF kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu (wa pili kulia) alipofika ofisini kwa mkurugenzi huyo kusaini kitabu cha wageni wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete (wa kwanza kulia).
Baadhi ya wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakishiriki kuchangia maoni wakati wa kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu amewataka watafiti wa programu ya Utafiti itakayoangalia huduma na ubunifu kwa watoto na vijana katika miji nchini Tanzania kutoa suluhisho la kudumu kuhusu mahitaji na usalama wa watoto na vijana ili kuwa na taifa lenye watoto wenye kujitambua.
Alisema ingawa anatambua kwamba tafiti zikifika mwisho wataitwa kuelezwa matokeo lakini kutokana na haja ya kutafuta suluhu ya changamoto zilizopo kwa sasa ni vyema watafiti wakapata muda wa kueleza maendeleo ya tafiti zao na hasa matokeo ya awali kabla ya kufika mwisho.
Alisema hayo katika kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana lililofanyika juzi kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji. Programu hiyo inaandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab).
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau takribani 40 kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi.
Alisema hali hiyo itasaidia Serikali kuchukua hatua mapema zaidi za kukabiliana na changamoto za watoto na hasa suala la malezi.
Alisema kwa sasa kumekuwa na changamoto nyingi za malezi na hivyo kusababisha uwapo wa watoto wengi kwenye mazingira magumu na pia mitaani.
Alisema utafiti unaokusudiwa ni utafiti wenye maana kubwa kwa kuwa unaangalia mazingira ya leo kwa manufaa ya taifa la kesho na kuondoa viashiria vya hatari katika malezi na hatima ya watoto wa Tanzania hasa wale wanaoishi mijini.
Alisema watoto na vijana wanaoishi mijini wanakabiliwa na changamoto nyingi na ni wajibu wa jamii kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinaondolewa kwa kuwepo kwa mbinu bora za kukabiliana na changamoto hizo, mbinu zenye manufaa na zinazowezekana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu warsha na programu ya tafiti inayoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na UNICEF alisema wanatengeneza programu hiyo kwa ajili ya kutanzua shida zinazowapata watoto na vijana wanaoishi katika miji.
Alisema warsha hiyo iliyojumuisha watafiti na wadau kadha wa masuala ya utafiti imelenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau ili kuweza kutengeneza programu mpya inayogusa masuala ya watoto na vijana katika miji yetu.
Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu kongamano hilo, alisema kwamba utafiti huo utafanywa chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) na kusema mipango miji ni suala muhimu kwa nchi ya Tanzania hasa wakati huu inapoelekea katika uchumi wa viwanda.
Alisema wakati Tanzania inatarajia kuwa na watu milioni 45 wanaoishi katika miji ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni nchi ya sita kwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu Duniani ifikapo mwaka 2050 na hivyo ipo haja ya kuwa na sera madhubuti inayohusu ulinzi kwa watoto na vijana wanaoishi mijini.
Alisema kutokana na serikali kutilia umuhimu wa masuala ya ukuaji wa miji katika Mpango wa Pili Miaka 5 wa Maendeleo 2016/17 - 2020/21 (FYDP II) kulianzishwa TULlab mwaka 2017 ambapo sekretarieti yake ni ESRF wakati mwenyekiti ni Wizara ya Fedha na Mipango.
Kazi ya TULab ni kuisaidia serikali katika masuala ya ukuaji wa miji Tanzania. Kwa kuzingatia tayari TULab imefanya tafiti na kuandaa Mpango Kazi kuelekea Maendeleo ya Miji.