HALIMA MDEE AKANA KUSHIRIKI MAANDAMANO


Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee amekana kushiriki katika mkusanyiko usio halali unaodaiwa kufanyika katika maeneo tofauti ya Buibui, Mwananyamala na barabara ya Kawawa Februari 16 mwaka jana kama inavyodaiwa na upande wa mashtaka.

Mdee ameeleza hayo jana Alhamisi Desemba 5, 2019 wakati akitoa ushahidi katika kesi ya jinai namba 112/2018 yenye mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi inayomkabili pamoja na wenzake.

Akiongozwa na wakili  wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa Februari 16, 2018 kabla ya mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa marudio jimbo la kinondoni alikuwa bungeni Dodoma.

Amedai  kuwa siku hiyo afya yake haikuwa nzuri na alishiriki mkutano huo kuonyesha mshikamano na upendo kwa mgombea na baada ya kushuka  jukwaani aliondoka.

Akijitetea mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, mbunge huyo amesema alikamatwa na askari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa anatokea Afrika Kusini kwenye matibabu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post