Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IGIP SIRRO AKUTANA NA MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA RELI TAZARA NA TRC

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amekutana na Menejimeti ya shirika la reli TAZARA pamoja na Menejimenti ya shirika la reli Tanzania TRC nakusema kuwa, hali ya usalama nchini imezidi kuendelea kuimarika kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na wadau wengine wa masuala ya usalama.

IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi na kutembelea vikosi vinne vilivyopo chini ya Jeshi hilo ikiwemo Kikosi cha Polisi Tazara, Reli, Ufundi pamoja na Kikosi cha Polisi Wanamaji.

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, ziara yake imelenga katika kufanya tathimini ya kiutendaji kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Makamanda pamoja na wasaidizi wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Tazara Bruno Ching’andu ameeleza kuwa, wameendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba ushirikiano huo umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu ikiwemo kuhujumu njia ya treni pamona na vitendo vingine vya rushwa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema kuwa, mbali ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo za baadhi ya watu kujihusisha na uhalifu lakini wameweza kudhibiti vitendo hivyo kutokana na ushirikiano uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com