Ukuaji wa teknolojia umekuwa chanzo cha uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na hii ni kutokana ya kila mmoja kutaka kuliteka soko sehemu mbalimbali hili linajihidhirisha kupitia brand mbalimbali za simu kama vile Infinix na nyinginezo, basi tujihakikishie haya nisemayo kupitia toleo jipya la Infinix S5.
Muundo wake
Infinix S5 imekuja na teknolojia ya kisasa kwenye kioo ambapo kamera yake ipo pembeni (hole-punch diplay) na hivyo kukifanya kioo cha simu kuonekana kwa ukubwa wake, tofauti na matoleo ya simu yaliyopita. Kioo cha simu kina ukubwa wa inchi 6.6 (uwiano wa 20:9), ambapo sasa utaweza kujinafasi zaidi unapoitumia.
Umbo la simu hii ni la plastiki na linapatikana katika rangi mbalimbali (Quetzal Cyan, Violent na Nebula Black). Ina sensa ya alama za vidole kwa nyuma ambayo inashikika kwa urahisi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taarifa zako.
Upande wa kushoto wa simu kuna sehemu mbili za kuweka laini (Nano-SIM cards), na sehemu ya kuweka memory vard (microSD) ya ukubwa hadi 256GB.
Vitufe vya kuongeza na kupunguza sauti vipo upande mwingine. Upande wa chini wa simu kuna tundu la spika (ear/headphones) na sehemu ya kuchomeka USB na chaja.
Boksi la simu linakuja na ‘cover’ la simu, ‘screen protector’ USB cable, kipini cha kutolea laini na chaja.
Kamera
Infinix S5 ina jumla ya kamera tano, ambapo kamera nne zipo nyuma ya simu, na moja ipo mbele.
Kamera kuu ya nyuma ya S5 ina ukubwa wa 16 megapixels (na aperture f/1.8 pamoja na PDAF). Mbali na hiyo kuna kamera yenye 5 megapixels ambayo inatumika kupiga picha za karibu. Pia kuna kamera nyingine yenye 2 megapixels ambayo inatumika kama sense kwa ajili ya picha (portrait mode), na kamera ya nne ni sensa kwa ajili ya mwanga (low light sensor).
Mbele ya Infinix S5 kuna kamera kwa ajili ya selfie yenye ukubwa wa megapixels 32, ambayo itakuwezesha kupata picha zenye ubora mkubwa. Hata hivyo unaweza kupunguza ukubwa huo hadi 16 megapixels ili kukuwezesha kupata picha isiyo na ukubwa (MBs nyingi) lakini yenye ubora.
Kiwango cha juu cha ubora wa video ni 1080p. Programu ya kamera (camera app) ina mfumo kukuwezesha kupiga picha bora kwa kutumia AI beauty system, ambapo mbali na hiyo kuna mifumo ya AR Stickers na Panorama, yote kwa ajili ya picha.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar Es Salaam, Wakiongea kuhusu ujio wa simu hiyo wameeleza vitu tofauti tofauti vilivyowavutia kwenye Infinix S5.
“Sijawahi kutumia Infinix katika maisha yangu, Ila hii S5 ina sifa nyingi zinazonishawishi kununua inatunza Sana chaji. Mara ya kwanza niliiona kwa mke wangu, Nikaanza kuitumia baada ya kupoteza simu yangu ya awali. Kuanzia hapo simu hii ilinishawishi sana kununua, Infinix nawaelewa sana najipanga na Mimi ninunue ya kwangu” Amesema Godfrey Ngimbo.
Kwa maelezo zaidi fika katika maduka yao yaliyopo Mlimani City, Posta na Kariakoo.
Social Plugin