Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 kutoka wilaya ya Budaka mashariki mwa Uganda, amemjeruhi mke wake vibaya baada ya mwanamke huyo kumchinja kuku aliyetakiwa kufanywa kitoweo kwenye siku kuu ya Krismasi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, bwana huyo alimnunua kuku kwa Sh15,000 za Uganda akipanga kumchinja siku ya Krismasi, lakini kwa bahati mbaya mke wake aliamua kumchinja na kumuandaa siku ya Jumapili tarehe 15 Disemba,2019.
Kwa mujibu wa katibu wa habari wa eneo hilo, Bw Joseph Gadimba, amesema baada ya mume kugundua kuwa kuku huyo hayupo tena, alimpiga mke wake na kumlaumu kwanini amemchinja bila ruhusa yake.
Bw Gadimba amesema ''alimpiga na kumchapa mke wake mara nyingi, huku akimuacha akipigania uhai wake.
Kwasasa mwanamke huyo anatibiwa katika kituo cha afya cha Budaka, mashariki mwa Uganda.
Wakazi wa eneo hilo walimtaka mwanaume huyo achukue majukuu yote yanayohusu matibabu ya mkewe ambayo alikubali kugharamia na kupelekea kesi hiyo kutoripotiwa polisi.
''Pale mwanamke huyo atakapo pona, ndugu zake kutoka eneo la Kapyani-Kasasira katika wilaya ya Kibuku, wanatarajia kufanya kikao na mwanaume huyo kujua chanzo cha yeye kumpiga mtoto wao na kutatua kesi hiyo,'' alisema Gadimba.
Chanzo - BBC
Social Plugin