Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema imepokea taarifa ya kuwepo kwa changamoto za mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha DSM (UDSM) na imeiagiza Bodi ya Mikopo na Uongozi wa Chuo kukutana na Serikali ya Wanafunzi UDSM (DARUSO) leo ili kutatua changamoto hizo.
Wizara imewataka Wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea na masomo wakati changamoto hizo zikishughulikiwa.
Kauli ya Wizara ya Elimu imekuja kufuatia Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM kutishia kwenda kukusanyika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), endapo saa 72 zitapita bila malalamiko yao kupatiwa ufumbuzi ikiwemo baadhi ya wanafunzi ambao ni wanufaika wa mkopo kutoingiziwa fedha.
Wizara imepokea taarifa ya kuwepo changamoto za mikopo ya wanafunzi wa UDSM. Imeiagiza Bodi ya Mikopo na Uongozi wa Chuo kukutana na DARUSO leo kutatua changamoto hizo.Wizara inawataka wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea na masomo wakati changamoto hizo zikishughulikiwa.— wizara ya elimu Tanzania (@wizara_elimuTz) December 16, 2019
Social Plugin