Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KITABU CHA MTOTO WA MIAKA 8 “BIBLIA YANGU” CHA ZINDULIWA KWENYE FURSA YA DAR

Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake
 MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda kulia akimkabidhi kitabu hicho Samweli mara baada ya kufanya uzinduzi
 MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso kushoto akimpatia nakala ya kitabu kilichoandikiwa na Mwanae Mtangazaji wa Kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM Radio Dkt Isaac Maro wakati wa uzinduzi huo
Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake na mdogo wake Alan Michael Gimeno


Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) katikati akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa kitabu chake


Jumamosi tarehe 7/12/2019  ilikuwa siku ya pekee wa mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) ambae alibahatika kuzindua kitabu chake cha kwanza ndani ya fursa ya Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Center

Kitabu cha BIBLIA YANGU kilizinduliwa na Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda

Samwel amekuwa mtoto wa pekee kwenye familia ambae Mungu Ameweka kipaji cha kuandika na kuchora na Sisi kama wazazi wake tumeamua kumsaidia ili kuiishi ndoto yake maneno hayo yamesema na mama mzazi wa Bi Suzana Senso

Kitabu cha kwanza cha Samwel kitakwenda Kuwa kinatolewa kwa watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya samwel kurudisha kwa watoto wezake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao ni mara chache sana kupata kitabu kinzuri na chenye hadithi za kwenye Biblia kutokana na mazingira wanayoishi maneno hayo yamesemwa na baba wa Samwel Bw Michael Samwel Gimeno

KAMPENI KALAMU YANGU
Ni maneno yatakayo kwenda kutumika kwenye  kampeni samwel ambayo itakuwa nikutembelee vituo vya  watoto yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na  kuwagawia vitabu ili nao waweze kusoma sio tu kusoma kitabu tu ila pia kusoma kitabu kilichoandikwa na mtoto mwezao

Kampuni hii inaanza mwezi huu wa 12 hadi siku ya wapendanao tarehe 14/2/2020 ambapo samwel atakwenda kula na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambacho tutakitaja siku zijazo na pia kuwagaia vitabu ya BIBLIA YANGU

Gharama ya kitabu itakuwa shilingi elfu 20,000 kuanzia 15/2/2020 baada ya kampuni ya KARAMU YANGU ukisha tarehe 14/2/2020

Mama Samwel alisema Kwa sasa tunatamani kupata watu wa ku support kutoa nakala ya  vitabu ambavyo tunatajia kuvigawa kwenye vituo vya watoto yatima Kwani hii kampeni haina mfadhili wa kufanya Ila ni wazazi tu  ndio tunaifanya na tunatamani kuwafikia watoto wengi sana
Kwa yeyote atakae wiwa kuungana nasi kwenye Hii kampuni anaweza ku wasiliana Kupitia namba 0736 372138

Tukiwa kama wazazi wa Samwel tunapenda kuwashukuru Joel Kiiya ambae ni  mentor wa Samwel, Bi Ezabel Simuyu ambae ndie ame design kitabu, photography wake Muki, Emanuel, Mkurungezi wa Fursa na wale waliotumia muda wao kufanikisha kitabu cha “BIBLIA YANGU” hadi kutoka.

MUNGU AWABARIKI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com