Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUBENEA AJITOA KUGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea ameandika barua ya kujitoa kugombea Umaakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, 2019 na kusema kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu anafaa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kuliko yeye.


Waliobaki kwenye nafasi hiyo ni Mbunge wa viti maalumu wa (Chadema), Sophia Mwakagenda  ambaye atachuana na mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu

Endapo wakiteuliwa  na baraza kuu la  chama kesho Jumanne Desemba 17, 2019 wawili hao wanatarajiwa kuchuana Desemba 18, 2019 katika mkutano mkuu wa chama utakaokuwa na ajenda ya kufanya uchaguzi wa kumpata mwenyekiti na makamu wenyeviti wa bara na visiwani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com