Wazazi wa mtoto aliyeuawa kwa kushambuliwa na kuku
Moja ya taarifa kutoka maeneo ya Malava Kaunti ya Kakamega nchini Kenya zinasema Kuku aliyemuua mtoto wa miezi 6 ameshambuliwa hadi kufa na wanakijiji wa eneo hilo.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo alifariki nyumbani kwao kwa mshtuko baada ya kushambuliwa na kuku ambaye alikuwa anajaribu kuwalinda vifaranga vyake.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na tovuti ya The Standard, Mama wa mtoto huyo aitwaye Robai Toboko amesema, familia imebaki na majonzi kwa mtoto wake huyo wa miezi 6 kufariki akiwa mikononi mwake .
"Nilikuwa nimempakata mwanangu, katika ile harakati yake kujaribu kumkamata mmoja wa vifaranga, kuku huyo alimrukia mtoto kwa hasira na kumgonga usoni na bawa lake. Mtoto alishtuka na akaanza kulia kwa muda mrefu kisha akapoteza fahamu" ameeleza mama wa mtoto
Aidha amesema mtoto wake alikuwa yupo vizuri kiafya ila alikata roho baada ya kupata mshtuko wa kushambuliwa na kuku, pia majirani walijitokeza kumsaidia japokuwa walikuwa wamechachelewa lakini walimuua kuku huyo pamoja na vifaranga vyake.
Social Plugin