Na Salvatory Ntandu - Shinyanga
Imebainishwa kuwa Kukosekana kwa kamati za maadili kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya Umma mkoani Shinyanga kumetajwa kusababisha ya migororo baina ya viongozi wa taasisi hizo na watumishi wao hususani katika utoaji wa haki pindi kwa mtumishi anapokosea au kwenda kinyume na sheria za utumishi wa umma.
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu mkuu wa kanda ofisi ya Rais, Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Gerald Mwaitebele, wakati akitoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za maadili kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na sheria ya maadili ya viongozi wa Umma yaliyofanyika mjini Shinyanga.
“Kamati hizi zipo kwa mujibu wa sheria, niwatake wakuu wa taasisi na Mashirika ya umma kuanzisha kamati hizi sambamba na kuzihuisha ambazo zimemaliza muda wake ili kutoboresha utendaji kazi kwa watumizishi ambao mnawasimamia”,alisema Mwaitebele.
Mwaitebele alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa migongano ya kimaslahi baina yao na watumishi katika maeneo yao ya kazi kwa kwani kamati hizo zitaweza kujadili na kuzipatia changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi hususani wanakiuka maadili ya Utumishi wa Umma.
Awali akifungua mafunzo hayo Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela aliwataka wakuu wa mashirika na taasisi za umma kufanya kazi kwa weledi pasipo kupendelea na kuepuka vitondo vya rushwa ambavyo vinaweza kukwamisha utendaji kazi wa shughuli za umma katika maeneo yao ya kazi.
“Nitoe rai kwa viongozi wote wa mashirika ya umma mkoani Shinyanga hakikisheni mnaziunda kamati hizi ili kuepuka migogoro ya kimaslahi ambayo ndio chanzo za ukwamishaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali za umma",alisema Msovela.
Mafunzo hayo yalilenga kuzikumbusha kamati za maadili za mkoa wa Shinyanga kuhusiana na sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.
Social Plugin