Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MABASI 15 YA ABIRIA KAHAMA YAFUNGIWA KUTOA HUDUMA YA KUSAFIRISHA ABIRIA

Na Salvatory Ntandu - Kahama 

Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria 102 yanayokwenda mikoani ambapo 15 yamefungiwa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria  65 yatozwa faini na 22 yakionywa baada ya kubainika kuwa na hitilafu mbalimbali ikiwemo kukosa breki, spiringi kufungwa kamba za katani jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa abiria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika oparationi maalumu ya ukaguzi wa magari iliyofanyika wialayani humo Mkuu barabarani nchini, Naibu Kamishina wa jeshi la Polisi, Ahmada Abdala Hamis amesema oparationi hiyo imelenga kukomesha ajali za barabarani hususani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

“Uzoefu unaonesha kipindi cha mwisho wa mwaka ajali nyingi hujitokeza kutokana na taama ya fedha zinazofanywa na baadhi ya wamiliki wa vyombo hivi ambao hudiriki kuigiza barabarani magari mabovu ili waweze kupata fedha bila kujali usalama wa abiri wao” alisema Naibu Kamishina Hamis.

Alisema Jeshi hilo limeongeza ukaguzi wa magari yote nchini ili kuhakikisha wanazuia ajali ambazo husababisha watanzania wengi kuteza maisha kutokana na uzembe wa madereva na wamiliki wa mabasi hayo ambao wengi wao huwa na tama za kujipatia fedha.

Katika hatua nyingine Kamisha Ahmada amelazimika kuzuia kuendelea na safari kwa basi la kampuni ya frester  investiment lilokuwa likisafisha abiria 60 kutoka Dar es laam kwenda Bukoba baada ya kubainika springi za gari hilo kufungwa mipira na kuagiza wabadilishiwe gari lingine.

Kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Safia Jongo amewataka madereva kutoendesha vyombo vya moto huku wakijua wazi kuwa ni vibovu na badala yake warekebishe hitilafu hizo  ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Nao Baadhi ya abiria wa basi la kampuni ya fresta investiment ambao walikumbwa na kadhia hiyo Mohamed Hassan na Adela Mbecha wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuyazuia magari hayo kusafiri huku wamiliki wake wakijua kuwa ni mabovu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com