Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJINA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2020


Wanafunzi 701,038 sawa na asilimia 92.27 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 wamechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza mwaka 2020.


Wanafunzi  58,699 hawajapata nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa huku ikiagizwa ujenzi wa madarasa ufanyike mapema ili waweze kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 5, 2019 Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amesema waliokosa nafasi wanatoka katika Mikoa 13 nchini huku Mkoa wa Kigoma ukiwa na idadi kubwa ya wanafunzi 12,092. 


“Wanafunzi 701,038 sawa na asilimia 92.27 watajiunga moja kwa moja kidato cha kwanza Januari 2020 na kati yao  wanafunzi 3,145 sawa na asilimia 0.41 watajiunga na shule za bweni.”

“Kati ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wavulana ni 335, 513 na wasichana ni 365, 525,” amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema hadi Februari 2020 madarasa yawe yamekamilika ili wanafunzi wajiunge mapema shuleni.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com