Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA ASILI MALINGITA AMEFARIKI DUNIA



Msanii Malingita enzi za uhai wake
Msanii Malingita akitoa burudani enzi za uhai wake
Msanii maarufu wa nyimbo za asili kutoka Kanda ya Ziwa Malingita Ng'wanasese amefariki dunia. 

Taarifa za kifo cha Msanii Malingita zimethibitishwa na mpwa wa marehemu, Msanii Mchele Mchele wakati akizungumza na Malunde 1 blog. 

“Ni kweli Mjomba wangu Malingita amefariki dunia usiku wa kuamkia le Jumatatu Desemba 2,2019. Alikuwa anaumwa tumbo na kifua kwa muda mrefu.Amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita mkoani Geita. 

Mchele Mchele amesema mazishi ya marehemu Malingita yatafanyika kesho Jumanne Desemba 3,2019 nyumbani kwake katika kijiji cha Bugarama kata ya Bugarama wilayani Geita.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Msanii Malingita. Amina.


Nimekuwekea hapa baadhi ya nyimbo za Msanii Malingita 




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com