Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakazi wa mikoa 15 nchini kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayotarajia kunyesha.
Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Ijumaa Desemba 20, 2019 imeitaja mikoa hiyo ambayo mvua hizo zinatarajia kunyesha kesho Jumamosi ni; Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Zanzibar.
Social Plugin