Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU SITA WAFARIKI DUNIA, 30 HAWAJULIKANI BAADA YA MAKAZI YAO KUSOMBWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO UGANDA

Picha ya maporomoko yaliyotokea mwaka 2010, nchini Uganda.

Watu sita wamefariki na watu wengine zaidi ya 30 hawajulikani waliko baada ya makazi yao kusombwa na maporomoko ya udongo katika wilaya ya Bududa, Mashariki mwa Uganda.

Karibu kila mwaka, watu wengi hupoteza maisha baada ya makazi yao kusombwa na maporomoko ya matope katika wilaya ya Bududa, Mashariki mwa Uganda.

Watu wapatao 30 bado hawajulikani walipo baada ya mkasa huo.

Kiongozi wa juu wa eneo hilo ameviambia vyombo vya habari kuwa watu kadhaa bado wamefukiwa na mwili mmoja pekee umepatikana mpaka sasa.

Hata hivyo, Kamishna kutoka idara ya kukabiliana na majanga, Martin Owur, amenukuliwa akisema miili mitatu imepatikana Bududa na mingie mitatu katika wilaya ya jirani Sironko, huku watu 47 wakiwa hawajulikai walipo na nyumba 38 zikiwa zimeharibiwa.
Barabara nyingi za Bududa zimefurika maji, hali inayofanya zoezi za uokoaji kuwa gumu.

Maporomoko ya matope yalifuatiwa na mvua kubwa iliyonyesha mfululizo kwa saa tano.

Serikali bado inafanya juhudi ya kuwahamisha watu 140 katika vijiji vipya.

Mwaka jana, watu 51 walipoteza maisha na zaidi ya watu 850 walikosa makazi baada ya maporomoko hayo kukumba eneo hilohilo.

Mvua kubwa isiyo ya kawaida katika eneo la Afrika Mashariki iliwaua watu zaidi ya 200 na zaidi ya watu milioni moja wengine. Nchini Kenya, zaidi ya watu 130 wamepoteza maishaa kutokana na mafuriko yaliyotokea tangu mwezi Oktoba.

Watabiri wa hali ya hewa wameonya kuwepo kwa mvua kubwa mpaka mwishoni mwa mwezi Disemba.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com