Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia
Kabaka akizungumza wakati akifungua Mashindano ya Wakina mama yaliyopewa jina la Kumekucha akina mama wa Musoma 2019
Mlezi wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni Mdhamini wa Mashindano hayo akizungumza wakati wa ufunguzi
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia Kabaka kulia akifuatilia mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara Wegesa Hassan |
Wadhamini wakiwa na washindi wa kwanza, kutoka kushoto watatu ni Naibu Meya wa Musoma mjini Mr. Igwe na wanne kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uhuru Hospitali Derick Nyasebwa |
moja kati ya mechi zikiendelea uwanjani |
Mlezi wa Chama cha mchezo wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni Mdhamini katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo |
Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama Gaudesia
Kabaka katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo mjini Musoma wa pili kulia ni Mlezi wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso ambaye pia ni Mdhamini mashindano hayo kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara Wegesa Hassan
NA MWANDISHI WETU, MUSOMA
MASHINDANO ya Wakina mama yaliyopewa jina la Kumekucha akina mama wa Musoma 2019 yamekuwa kivutia kukibwa Musoma Mjini huku waaandaji wakihaidi kuendelea
kuyafanya kila mwaka lengo kutoa fursa kwa wanawake kuonyesha vipaji vyao kupitia huko.
kuyafanya kila mwaka lengo kutoa fursa kwa wanawake kuonyesha vipaji vyao kupitia huko.
Mgeni rasmi kwenye mashindano hayo alikuwa Mama Gaudesia
Kabaka Mwenyekiti wa UWT Taifa ambapo alipongeza waandaaji wa mashindano
hayo na kusema hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kutokea Mara
Kwani haijawahi kutokea na yameendeshwa kwa kufuata kanuni za mashindano
kwa michezo.
Michezo ambayo ilifanyika kwenye mashindano hayo ni Netball, wakina mama kukimbiza kuku, kuvuta kamba na kukimbiza magunia ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha tunaendelea vipaji vya wakina mama.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Mlezi wa Chama cha mchezo
wa Netball Mkoani Musoma mjini Wakili Suzana Senso alisema kwamba
wameamua kuandaa mashindano hayo kwa sababu wakina mama wanakuwa wamesahaulika kwenye michezo hasa Netball.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo Mlezi wa Chama cha Mchezo wa Netball mkoani Musoma Wakili Suzana alisema kwamba alisema wameamua kuanzisha mashindano hayo ili kutoa fursa kwa wakina mama nao kuweza kuonyesha vipaji vyao walivyonavyo.
“Kikubwa zaidi niwaambie kwamba tumeamua kufanya mashindano hayo kwa wakina mama waweze kuonyesha vipaji vyao kwani mabonanza mengi hayausishi wakina mama hilo ndilo ambalo limewasukuma kuwasiliana na
Naibu Meya wa Musoma Mjini Bwana Igwe na tukaona tuandae hicho kitu
tunamshukuru Mungu kimekwenda vizuri”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba pia wana mpango wa kuandaa mashindano mengine ya wakina mama yatakayofanyika Machi 8 mwakani lengo kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha kushiriki kwenye mashindano mbalimbali nao waweze kuendeleza vipaji vyao.
Hata hivyo aliyashukuru makampuni mbalimbali yaliyojitokeza kuunga mkono mashindano hayo kwa kuyasaidia ambao ni Uhuru Hospitali, Chama cha Netbally Mkoa Musoma na Meya wa Manispaa Musoma, UWT Mkoa.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhuru Hospitali Dkt Derick Nyasebwa alisema kwamba wameamua kushiriki mashindano hayo ya wakina mama na wamefurahi kwa sababu yeye pia ni mzaliwa lakini kwa niaba ya Uhuru Hospitali .
Alisema waliamua kuhakikisha wanashiriki kwenye michezo hiyo kwani kufanya hivyo ni kampeni kubwa zinazoendelea nchini kutoka wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto inayoongozwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuhakikisha wanaelimisha watu kuepukana na magonjwa yasiyoambuliza kupitia michezo ni njia nzuri ya kuepukana na kusukari,saratani na msukumo wa damu kuwa juu.