Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBOWE ADAI KUANZIA MWAKA 2020 CHADEMA HAITATEGEMEA TENA RUZUKU KUJIENDESHA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimezindua mfumo wake mpya wa Kidigitali wa uendeshaji wa Chama hicho ambapo kitakuwa kikikusanya ada za Uanachama wa wanachama wake na kukifanya kujitegemea.


Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama  hicho uliofanyika leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, amesema mfumo utawasaidia kukusanya karibia Bilioni 15 kwa mwaka.

Mbowe amesema programu hiyo iliyozinduliwa leo Jumatano Desemba 18, 2019 inahusisha uandikishaji wa wanachama kidigitali, kufanya mikutano kidijitali pamoja na kampeni.

“Kila mwaka mwanachama anatakiwa alipie Sh1,000 ya ada, kwenye vikao hivi tunapendekeza iwe Sh2,500 kwa mwaka. Maana yake ni nini? Leo hii chama kinapata ruzuku ya Sh3 bilioni kwa mwaka. Gharama ya kufanya mkutano wa baraza kuu ni zaidi ya Sh1 bilioni kwa hiyo ruzuku peke yake haitoshi.”

“Kupitia Chadema Digital tuna digital fund raising, tumekubaliana kuchangia Sh2,500. Asilimia 90 wana Chadema wana simu za mkononi, kila mwanachama akilipa kwa simu tutapata Sh15 bilioni kwa mwaka.”

Amesema kupitia vikao vyao wataibadilisha katiba ya Chadema ili kuruhusu mfumo huo ufanye kazi vizuri, “tunahitaji kujenga chama cha kujitegemea na hili msajili usikie, maana yake kuna watu wanafikiri chama kinategemea sana ruzuku.”

Amesema kutokaa na mfumo huo, chama hicho sasa hakihitaji tena kufanya mikutano ya hadhara ili kupata wanachama wapya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com