Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MDOGO WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA, SETH BOSCO AFARIKI DUNIA



Mdogo wa Marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco amefariki usiku wa kuamkia leo Desemba 07, 2019 nyumbani kwao Mbezi Temboni. Msiba upo Mbezi Temboni kwa mama yake Kanumba.  Abela (Dada wa Marehemu) amethibitisha.



“Mdogo wangu Seth alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye uti wa mgongo akafanyiwa upasuaji na tukawa tunamuuguza nyumbani kwa Mama hapa Kimara Temboni, Jana jioni akalalamika maumivu yanazidi tukampeleka Muhimbili akapata afadhali tukarudi nae nyumbani



“Tuliporudi nyumbani kutokea Muhimbili alikuwa yuko vizuri tu, akaomba alale kidogo kisha tumuamshe aangalie TV kuna kipindi anakipenda, akiwa kitandani akafariki, tulikuwa na Daktari nyumbani anasema Seth alipata shida ya kupumua, pumzi zilimuishia



“Mwili wa Seth kwa sasa umehifadhiwa Muhimbili na shughuli zote za Mazishi zinafanyika hapa Kimara Temboni DSM, nyumbani kwa Mama Kanumba” - Amesema Abela (Dada wa Maremu)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com