Mvua zilizoanza kunyesha leo asubuhi ya Disemba 17, 2019, jijini Dar es salaam, zimepeleeka mafuriko katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo na kusababisha kadhia na kero mbalimbali kwa wananchi.
Kutokana na changamoto hiyo ya mvua vitu mbalimbali vimeonekana vikisombwa na maji hayo ikiwemo sofa huku watu mbalimbali wakijitolea kuwaokoa watoto kwa kuwavusha kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Mvua hiyo imetajwa kuathiri maeneo mengine ikiwemo :
1. Jangwani Kutokea fire kwenda Magomeni na Magomeni kwenda fire. Imefungwa.
2. Jangwani kwa nyuma kutokea Kariakoo to kigogo imejaa Maji.
3. Umoja wa mataifa. Kutokea Almuntazir mpaka Muhimbili primary kumajaa Maji.
4. Scout upanga barabara ya malik pamejaa maji kuja junction ya Muhimbili
5. Barabara ya Fire hapa katika hospitali ya Regency pamejaa Maji
6. Kamata ktk barabara ya nyerere katika fly over ya treni pamejaa Maji
7. Kamata kutokea kariakoo kuja barabara ya nyerere pamejaa Maji.
8. Waterfront hapa kuja central police pamejaa Maji
9. Barabara ya Mwamnyange kuja main road ya barabara ya whitesand pamejaa Maji
10. Barabara ya Whitesand kuja round about ya whitesand hali si shwari
11. Basihaya kuja Nyaishozi hali sio nzuri
12. Junction ya barabara ya gonna katika Mataa Maji yamejaa
13. Mbozi road Chang'ombe Maji kuna maji ya kutosha
14. Junction ya hapa kwa sokota napo pamejaa Maji
15. Sinza Legho darajani hapa pamejaa maji pia
16. karibu na ofisi za kiwango kuna daraja nalo limejaa maji ya kutosha litanata kutema kabisa, huko Mburahati, Kigogo ni mwendo wa mafuriko tuu maji yamejaa ndani, ukija hapo mkwajuni kwenye mto napo pamejaa maji yamepita mpaka barabara
Social Plugin