Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWALIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA KULAWITI WATOTO WADOGO


Mkuu wa Wilaya wa Iringa Mjini, Richard Kasesela amesema polisi wilayani humo inamshikilia mkazi wa Semtema, Anord Mlay ambaye ni mwalimu kwa tuhuma za kulawiti watoto wadogo 24.



Imeelezwa kuwa wengi wa watoto hao ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika eneo hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa watoto hao wanadaiwa kulawitiwa katika kipindi cha miaka mitatu na na mtuhumiwa huyo.

Akizungumza na wananchi wa mtaa huo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alieleza akushtushwa na ukubwa tatizo hilo na kuamua kuchukua hatua ikiwamo kuunda kamati ya watu 10 kwa ajili ya kufuatilia na kubaini watoto ambao wamefanyiwa ukatili huo.

Kasesela alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na michezo ya kompyuta, na kwamba alikuwa akiwarubuni watoto kwa zawadi ndogo ndogo zikiwamo fedha.

Kasesela alifafanua zaidi kuwa Mlay pia alikuwa akiwatishia watoto kuwatoa uhai ikiwa wangeruhusu mtu mwingine kujua suala hilo.

Alisema alieleza kuwa uchunguzi dhidi ya mtuhuhiwa huyo ukikamilika, atapelekwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Kasesela, Mlay ni mwalimu ambaye alihitumu katika Chuo Kikuu cha Iringa, na anamiliki kituo chake cha kuchezesha michezo ya kompyuta kwa watoto wadogo katika mtaa wa Semtema ‘A’.

Kasesela  pia aliwataka wazazi na walezi katika Manispaa ya Iringa kuwa makini na watoto wao wanaocheza michezo katika vituo vya watoto maarufu pamoja na kuwataka kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwafichua wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com