Mwanachama mkongwe wa klabu ya Yanga Ibrahim Omary Akilimali amefariki dunia leo asubuhi ya Desemba 14,2019 katika Hosptali ya Bagamoyo baada ya kuugua Kwa muda mrefu.
Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti Umoja wa Tawi la Yanga kwa Mtogole, Waziri Ramadhani amesema marehemu Akilimali ambaye aliwahi kuwa katibu wa Baraza la Wazee Yanga, atazikwa kesho saa 10 katika Makaburi ya Tandale kwa Mtogole.
Social Plugin