Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier Q400, iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada imekwishaachiwa huru.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo Desemba 12, 2019, Jijini Mwanza, wakati akifungua semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
"Kwanza kwa taarifa tu Ndege yetu iliyokuwa imeshikwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokea hapa hapa Mwanza" amesema Rais Magufuli.
Taarifa za kukamatwa kwa Ndege hiyo zilitolewa siku ya Novemba 23, 2019, Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
==>>Msikilize hapo chini
Social Plugin