Moja ya mambo yaliyovutia na kushangiliwa sana na wananchi kwenye sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana na miaka 57 ya Jamhuri, ni miondoko ya ndege vita na onesho la makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wakishuka kwenye Helkpta za Kijeshi.
Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, zilipambwa na nyimbo, ngoma za jadi na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kutoka Mkoa wa Mwanza na mikoa mingine nchini.
Kama mchezo wa kwenye filamu, maonyesho ya ndege za kivita yalianza kwa ndege tatu kupita kwa kasi juu ya anga na kuibua shangwe kutoka kwa viongozi na wananchi waliokuwa uwanja wa CCM Kirumba
Kasheshe likaja baada ya ndege za kivita zenye miungurumo ya vishindo zilipoanza kukatiza angani na kuzua hofu kwa baadhi ya wananchi waliojikuta wakishindwa kuhimili vishindo hivyo na kuzimia kwa hofu. Baadae lilifuata zoezi la Makomandoo wa JWTZ Kushuka Kwenye Helkopta za Kijeshi kwa kutumia Kamba
VIDEO: Ndege za kivita kadhalika ndege ya heshima zikipita mbele ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk John Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. #SherehezaUhuru58 pic.twitter.com/x4vc2rrrKO— MPEKUZI (@mpekuzihuru) December 9, 2019
Social Plugin