Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania ‘Tanzania Police Female Network’ wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Benki ya CRDB tawi la Shinyanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 3.5 katika Kituo cha kulelea watoto wenye ualbino Buhangija Jumuishi,Kituo cha Kulelea wazee cha Kolandoto,Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha afya Kambarage.
Miongoni mwa vitu vilivyotolewa leo Desemba 12,2019 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni pamoja na mchele,unga,sukari,mafuta ya kupikia,mafuta ya kujipaka,sabuni,viberiti,miswaki,dawa za meno,viatu,taulo laini ‘pedi’,kalamu na soda.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vitu hivyo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga,amesema polisi wanawake wameamua kushirikiana na Benki ya CRDB kutafuta mahitaji muhimu kwa ajili ya watoto wenye ualbino,wazee na wagonjwa ili kuonesha kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanawajali.
“Tumeguswa na maisha ya watoto wenye ualbino lakini pia wazee hawa kwani wanaonekana kama wanatengwa na jamii,mfano watoto hawa wenye ualbino baadhi yao wamebaki hapa Buhangija baada ya shule kufungwa,hivyo tumewapatia mahitaji muhimu ili kuonesha kuwa jamii ipo pamoja nao na inawapenda”,amesema Salia.
Salia ametumia fursa hiyo kuikumbusha jamii kuwapenda watoto na wazee na kuepuka kuwatenga kwani wana haki sawa na watu wengine katika jamii.
Polisi wanawake wakiwa wameambatana na maafisa kutoka Benki ya CRDB wametembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiweko kula keki na watoto kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Jumuishi ambacho sasa kina watoto 230 (wenye ualbino 131,wasioona 25 na viziwi 74) na kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto chenye jumla ya wazee 12.
Aidha wametembelea wodi za akina mama,watoto na wazazi na kuwapatia zawadi wazazi na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kituo cha afya Kambarage.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga akizungumza katika kituo cha Kulelea watoto wenye uhitaji cha Buhangija Jumuishi kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Desemba 12,2019 wakati polisi wanawake walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema wameamua kufika Buhangija Jumuishi ili kuwatia moyo watoto wenye ualbino,wasioona na viziwi kwamba jamii ipo pamoja nao.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buhangija,Selemani Kipanya akiwakaribisha polisi wanawake na Benki ya CRDB. Alisema hivi sasa kituo cha Buhangija Jumuishi kina watoto 230 (wenye ualbino 131,wasioona 25 na viziwi 74).
Afisa kutoka Benki ya CRBD,Lewis Temu akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji cha Buhangija Jumuishi ambapo alisema wameguswa na hali ya maisha ya watoto hao na kuamua kushirikiana na polisi wanawake kutafuta zawadi/mahitaji kwa ajili ya watoto hao.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga Victoria Maro akizungumza katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Sehemu ya zawadi zilizotolewa na Polisi wanawake wilaya ya Shinyanga na Benki ya CRDB kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia na maafisa kutoka Benki ya CRDB Lewis Temu na Getrude Ikongo wakikabidhi sukari kwa Mwalimu Selemani Kipanya (kushoto) na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Zoezi la kukabidhi sukari likiendelea. Vitu vingine vilivyokabidhiwa kwa watoto hao ni pamoja na unga,mchele,sabuni,dawa za meno,miswaki,viatu,mafuta ya kupikia,sabuni,juisi,soda,taulo laini 'pedi',biskuti n.k.
Askari polisi wakicheza na watoto katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Mtoto akitoa neno la shukrani kwa zawadi zilizotolewa na polisi wanawake na benki ya CRDB.
Mtoto akikata keki iliyoandaliwa na polisi wanawake na benki ya CRDB kama ishara ya upendo kwa watoto waliopo katika kituo cha Buhangija Jumuishi.
Zoezi la kukata keki likiendelea.
Mtoto akimlisha keki Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akimlisha keki mtoto.
Afisa kutoka Benki ya CRDB Lewis Temu akimlisha keki mtoto.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akimlisha keki mtoto.
Afande Stella akimlisha keki mtoto.
Afande Amina akimlisha keki mtoto.
Afande Vivian Zabron akimlisha keki mtoto.
Afande Tumaini aliyeambatana na polisi wanawake akimlisha keki mtoto.
Polisi wanawake,maafisa wa benki ya CRDB na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakipiga picha ya pamoja na watoto.
Askari Polisi wanawake wakiwa katika kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga walipotembelea kituo hicho na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akiwaelezea wazee wa Kolandoto lengo la ziara yao kwenye kituo hicho.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia na Afande Amina wakikabidhi zawadi ya dawa za meno kwa Mwenyekiti wa Wazee Kolandoto,Samora Maganga.Vitu vingine walivyokabidhiwa wazee hao ni pamoja na sabuni,mafuta ya kupikia,mafuta ya kupaka,unga,mchele n.k.
Kaimu msimamizi wa kituo cha Kolandoto,Godbetha Kacharuzi akitoa neno la shukrani kwa msaada uliotolewa na polisi wanawake na benki ya CRDB.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akiagana mmoja wa wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto.
Askari polisi wanawake wakiondoka katika kituo cha kulelea wazee cha Kolandoto.
Polisi wanawake wakiwasili katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kusalimia akina mama katika wodi ya wanawake waliojifungua.
Polisi wanawake wakiwa katika wodi ya akina mama waliojifungua kwenye kituo cha afya Kambarage kwa ajili ya kutoa zawadi ya sabuni na taulo laini 'pedi'.
Afisa kutoka Benki ya CRDB Getrude Ikongo akitoa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage.
Polisi wanawake wakitoa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage.
Zoezi la kutoa zawadi likiendelea wodini.
Polisi wanawake na maafisa wa benki ya CRDB wakimpongeza mama aliyejifungua katika kituo cha afya Kambarage.
Askari polisi akiwa amebeba mtoto aliyezaliwa katika kituo cha afya Kambarage.
Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu katika kituo cha afya Kambarage akiwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro (wa pili kulia), na Meneja Biashara Benki ya CRDB Mwanahamisi Idi (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia.
Polisi wanawake wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na maboksi ya zawadi mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa na akina mama wajawazito na waliojifungua.
Polisi wanawake wakielekea katika wodi za watoto na wanawake katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakielekea katika wodi za watoto na wanawake katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua kwa njia ya kawaida katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua kwa njia ya kawaida katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa katika wodi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya kawaida.
Afande Mariam akitoa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa mama aliyejifungua katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akitoa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa mama aliyejifungua katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua kwa njia ya kawaida.
Polisi wanawake wakiwa nje ya wodi ya akina mama.
Polisi wanawake wakiwa ndani ya wodi ya akina mama.
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake wilaya ya Shinyanga,Grace Salia akiteta jambo na Meneja Biashara Benki ya CRDB Mwanahamisi Idi (kulia).
Polisi wanawake wakiwa katika wodi ya watoto.
Zoezi la kugawa zawadi likiendelea katika wodi ya watoto.
Mtoto akipokea zawadi ya sabuni.
Polisi wanawake wakitoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga baada ya kugawa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa wagonjwa na akina mama waliojifungua.
Polisi wanawake wakitoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga baada ya kugawa zawadi ya sabuni na taulo laini kwa wagonjwa na akina mama waliojifungua.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin