Serikali imesema inapanga kununua ndege ya mizigo itakayosafirisha shehena ya bidhaa za maua na mbogamboga kwa lengo la kuongeza fursa za uwekezaji na biashara kwa wakulima nchini.
Mapango huo unaokusudia kuongeza na kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa njia ya anga ndani na nje ya Tanzania utawezesha safari za moja kwa moja za bidhaa hizo kwenda na kutoka nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Rais Magufuli jana Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati wa shughuli ya mapokezi ya ndege aina ya Bombardier Q-400
Alisema mikakati hiyo ndiyo maana Serikali inajenga vyumba vya barafu vya kuhifadhi maua na mbogamboga katika uwanja wa Mwanza, Songwe na Mbeya.
Social Plugin