Piobbico Itali: Kijiji kinachowasherehekea watu wenye sura mbaya zaidi duniani
Kijiji kimoja kinachofahamika kama Piobbico kimekuwa maarufu kwa kuwa na watu wenye sura mbovu zaidi duniani na kwa sasa dhana hiyo imekifanya kuwa maarufu zaidi duniani.
Kijiji hicho ambacho kimekuwa kikienzi utamaduni huu kwa miaka 140 sasa, kiko katikati ya milima ya Apennine na bahari ya Adriatic katikati mwa Italia.
Piobbico ni kijiji cha zamani kilichozungukwa na majengo ya matofali na misitu iliyostawi. Lakini licha ya muonekano wake wa kuvutia, kijiji hicho kinafahamika sana kwa kuwa na watu wenye sura mbaya zaidi duniani.
Tangu mwaka 1879, kijiji hichi chenye watu karibia 2,000 kiliunda chama kwa jina ''Club Dei Brutti'' cha watu wa kutisha na kinaamini kwamba ''mtu ni vile alivyo wala siyo vile anavyoonekana''.
Wazo hilo lilianza zamani na kuchukuliwa kama wazo la kawaida tu lakini limegeuka na kuvutia ulimwengu kiasi kwamba watu wengine wanaomini kwamba wanasura mbaya zaidi pia nao wanatuma maombi ya kutaka kujiunga na chama hicho.
Wakati huu, chama hicho kinajumuisha watu karibia 30,000 kote duniani.
Namna ya kujiunga na chama chenye watu wa sura mbovu zaidi duniani
Chama hicho cha Club Dei Brutti awali kiliundwa kwa ajili ya wanawake wasio na wachumba.
Lakini kadiri siku zilivyoendelea kusonga mbele, wanavijiji walichukua jukumu na kukumbusha jamii kwamba uzuri wa ndani ni muhimu zaidi kuliko unaoonekana kwa nje na mwaka 2007, kijiji cha Piobbico kikazindua kinyago kwa ajili ya watu wenye sura mbaya kwenye eneo hilo.
Leo hii, ni rahisi kabisa kwa mtu kujiunga na chama hicho. Wachohitajika kufanya wanachama waandamizi ni kuchagua sura
Ya anyetaka kujiunga kama ni mbaya kiasi cha kurudhisha
Na kutazama watakuweka katika kundi gani. Makundi yamegawanywa kuanzia lile la kutisha kidogo hadi la watu wanaotisha kisawa sawa
Hata hivyo chama hicho kimeamua kutojikita zaidi katika ubaya wa sura badala yake kuangalia uzuri wa moyoni bila kujali kile watu wanachokifikiria kukuhusu.
Jumapili ya kwanza ya Septemba 2019, wanachama kutoka kila pembe ya dunia walikusanyika katika kijiji cha Piobbico kwa ajili ya tamasha la mtu mwenye sura mbaya zaidi duniani na kumchagua rais wa chama hicho, wakasajili wanachama wapya na kula vyakula vya eneo kama vile kuvu, aina ya ugali na tambi.
Katika nchi ambayo inatilia mkazo zaidi kuhakikisha unaonekana mzuri, kijiji hiki kinathibitisha kwamba mtu anatakiwa kujithamini vile alivyo na kufurahia uhalisia bila kujali ubovu wa sura mbako vilevile, bado kutavutia wengi.
Chanzo - BBC
Social Plugin