Na Alex Sonna, Chemba.
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya JUAN, inayotekeleza mradi wa Maji wa Kelema Kuu, katika Kijiji Cha Kelema Balai Wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, kuhakikisha ndani ya siku kumi mradi huo uwe umekamilika.
Mradi wa Maji wa Kelema Kuu wenye thamani ya shilingi milioni Mia mbili ishirini na tatu,(milioni 223) na ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2014 na ulikamilika lakini ikitoa maji zaidi ya wiki mbili tu, kwa kutandikwa mabomba yakiyochini ya kiwango na kuamuriwa mkandarasi huyo kutandika mabomba mengine yenye viwango.
Mkuu huyo wa TAKUKURU ametoa maagizo hayo Mara baada ya kutembelea mradi huo na kuagiza ndani ya siku kumi mradi huo uwe umekamilika na wananchi waanze kupata huduma ya maji Safi na salama ambayo wameikosa kwa mda mrefu.
“Tumetoa siku hizo kumi kwa hawa wakandarasi wakamilishe kwa sababu mvua zikizidi watapata visingizio na Kama unavyoona Kuna sehemu wamechimba na Kutokana na mvua mtaro unafukiwa na tope,” amesema Kibwengo.
Akitoa ufafanuzi baada ya kufanya uchunguzi wao amesema walichokibaini ni kwamba yaliyonunuliwa kuweka katika mradi huo yenye PN 6 badala ya 12.5 kama zilivyoidhinishwa katika mkataba wa kutekeleza mradi hio.
Amesema siku hizo walizotoa hakutakuwa na msamaha wowote kwa kampuni hiyo kwasababu ni uzembe na udanganyifu uliofanywa na mkandarasi huyo kinachotakiwa ni wao kufanya kazi jaraka iwezekanavyo hasa ukizingatia mitaro tayari imechimbwa.
Naye Mhandisi wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilayani Chemba Robert Mganga amesema kazi iliobakia ni nyepesi sana hivyo wiki moja inatosha kukamilisha kufanya utandikaji hio wa mambomba.
“Hakuna.kazi ngumu hapa sema hii kampuni inaleta uzembe,tuko nao pamoja hivi sasa kuhakikidha wanakamilisha,”amesema Mganga.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Ndoroboni amesema kitongoji hiko kina shida ya maji inayopelekea wakazi wa eneo hilo kuuafuata kijiji cha Kelema Balai kama mili mbili kutoka Kelema Kuu.
Ameiomba serikali kwa kishirikiana na serikali ya mtaa kusimamia mradi huo ukamilike wakazi waweze kupataaji safi kwa ajili ya matumizi yakila siku amesema wakazi wengine hudhindwa kwenda umbali mrefu na badala yake wanatumia maji ya mabwawa ambayo ni machafu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa kampuni ya Juan Mhandisi Inocent Benard amesema wakazi wa eneo hilo wategemee mwezi huu kupata maji kutokana na kuwa watakamilisha ndani ya siku ambazo wametakiwa kukamilisha.