Katibu Mkuu Wa Madini Prof. Simon Msanjila akichangia hoja wakati wa majadiliano |
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo |
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongoza Kikao na wataalamu
waliofanya tathmini ili kujiridhisha endapo Tanzania inakidhi vigezo vya
kupewa cheti ili kuwa miongoni mwa nchi zinazotekeleza matakwa ya Nchi
wanachama kwa kutokuruhusu rasilimali za nchi kutumika kuchochea maasi.
Na Nuru Mwasampeta, DSM
Imeelezwa
kwamba Kabla ya kuisha Mwaka huu wa Fedha 2019/2020 Tanzania itakuwa
imepata Cheti Maalumu kitakachoitambulisha kuwa ni nchi iliyokidhi
Vigezo vya nchi zinazotumia rasilimali zinazopatikana nchini yakiwemo
madini kutochochea machafuko kwa nchi wanachama za maziwa makuu.
Cheti
hicho kitaiwezesha nchi kutathmini na kutoa vibali kwa wachimbaji,
wauzaji na wasafirishaji wa Madini ya Bati (tin), dhahabu na Tangsten
kuuza Madini hayo nje ya nchi.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo tarehe 18
Desemba, 2019 jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kilicholenga
kupokea ripoti juu ya tathmini iliyofanywa kwa lengo la kujiridhisha
endapo Tanzania inakidhi vigezo vya kupewa cheti cha nchi wanachama
zilizokidhi matakwa hayo.
Ripoti
hiyo iliwasilishwa kwa Naibu Waziri Nyongo aliyeambatana na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjila na wataalamu kutoka viongozi wa
sekretariati ya Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Maziwa Makuu yenye jumla
ya nchi wanachama 12 ulioundwa kwa lengo la kulinda rasilimali
zinazopatikana katika nchi zao ili zisitumike katika kusababisha na
kuendeleza machafuko katika nchi wanachama.
Akizungumza
katika kikao hicho, Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alisema anatarajia
nchi za Rwanda, Uganda na Kongo zitafanya kazi kwa pamoja ili kuiwezesha
Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo kutokana na nchi
kukidhi matakwa muhimu ya kupewa cheti hicho.
Nyongo
alisema kuwa tathmini iliyofanywa na Sekretarieti Nchini kuanzia tarehe
13 hadi 18 Desemba, 2019 imeonesha wazi namna Serikali ya Tanzania
inavyoendesha biashara ya Madini na kuomba taarifa hiyo itumike
kuharakisha mchakato wa nchi kupewa cheti hicho.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka
wajumbe kukamilisha kazi hiyo kabla ya Mwaka kuisha ili kuiwezesha
Tanzania kupata cheti hicho Mapema iwezekanavyo.
Akizungumza
Namna mchakato wa tathmini hiyo ilivyofanyika, Gerard Nayuburundi
mmoja kati ya wataalamu waliofanya tathmini nchini kutoka Burundi
alisema wako tayari kuandaa kikao ili kuwasilisha na kujadili matokeo
waliyoyapata ili kuiwezesha Tanzania kupata cheti hicho.
Aliongeza kuwa, wamejiridhisha na namna Tanzania inavyolinda na kuwasaidia wawekezaji ili Uwekezaji wao nchini kuwa na m
tija.
Akizungumzia
namna tathmini hiyo ilivyofanyika Gerard alisema ilihusisha mahojiano
na Ukaguzi wa taarifa mbalimbali wa namna mchakato wa uchimbaji, uuzaji,
na usafirishaji wa rasilimali madini unavyofuata taratibu zilizowekwa
na nchi wanachama.
Mpaka
sasa ni nchi tatu tu za Uganda, Rwanda na Kongo zinazomiliki cheti
hicho ambapo Tanzania itakuwa nchi ya nne kupewa cheti hicho muhimu.
Social Plugin