Waamuzi wa mchezo kati ya Isimani fc na Young Stars kutoka kushoto ni Rajabu Luvanga katika ni Rashid Zongo (Shungu) na mwisho kulia ni Hashim Mbaga ambao wamekuwa wakichezesha mara kwa mara mashindano ya Asas Super League 2019/2020 mkoani Iringa
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Isimani Fc wakiwa kwenye furaha mara baada ya kutua hatua ya Nusu fainali ya Asas Super League 2019/2020
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
TIMU tatu zinazoshiriki Asas Super Leaguer 2019 zimekuwa timu za
kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali katika mashindano ya ligi soka daraja la
tatu mkoa wa Iringa,timu hizo ni Mafinga Academy ya mjini Mafinga, Ismani fc
na Kidamali huku wakiishubili timu moja kutoka kundi B ili kukamilisha
timu nne zinazotakiwa kuingia hatua ya nuru fainali.
Timu hizo ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ubingwa
msimu huu zimefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuongoza na nyingine kushika
nafasi ya pili kwenye makundi yao ambapo Mafinga wakiwa na pointi 9 na mchezo
mmoja mkononi huku Ismani kutoka kundi A wakifikisha pointi 10 na kufatiwa na
Kidamali wenye pointi 8.
Ligi hiyo ambayo imekuwa ya upinzani mkali hasa kwa kundi A
ambapo michezo ya mwisho ndio iliamua timu ambazo zimetinga nusu fainali baada
ya timu zote nne kuwa na pointi 7 kila mmoja kabla ya michezo iliyochzwa juzi
na kuzipa nafasi timu za Ismani Fc na Kidamali kutinga nusu fainali.
Wakati Ismani fc wakijihakikishia kuingia nusu fainali baada ya
kuwafunga Young Stars magoli 2 -1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Ismani kwa
magoli ya Mohamed Msigala na Razack Kibuga huku goli la Young Stars likifungwa
na Majaliwa Hussen.
Kwa upande wao timu ya Kidamali ilitinga hatua hiyo
baada ya kutoka sare ya goli 1 – 1 dhidi ya Kalinga kwa magoli yaliyofungwa na
mchezaji hatari Emanuel Geka wa Kidamali na goli la John Mbuna hivyo zote kuwa
na pointi 8 lakini Kidamali wakifuzu kwa faida ya magoli mengi ya kufunga.
Kundi B ambalo limeonekana limekuwa na upinzani mkali inasubili
mechi za mwisho kuweza kuamua timu ambazo zitaungana na Mafinga Academy kutinga
hatua ya nusu Fainali ambapo timu zote zilizobaki zina nafasi ya kutinga hatua
hiyo kutegemeana na matokeo ya michezo yao ya mwisho.
Timu ya soka ya Irole fc yenye pointi 8 itakutana na mabingwa wa
msimu uliopita Nzihi Fc katika mchezo utakaochezwa uwanja wa Irole ambapo
endapo ikishinda au kutoa sare itajihakikishia moja kwa moja kutnga hatua ya
nusu fainali na mchezo kati ya Mafinga Academy na Mkimbizi Fc utachezwa Mafinga
na Mkimbizi wakiibuka na ushindi atasubiri matokeo ya Nzihi na Irole hali
inayofanya michezo hiyo kuwa na upinzani mkali.
Ligi hiyo ambayo imekuwa na upinzani mkali msimu huu na
kudhaminiwa na kampuni ya maziwa ya Asas, bingwa ataondoka na Kombe, sh. 2,000,000,
Jezi seti moja, mipira 3, nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa na
Cheti cha Ushiriki wakati mshindi wa pili sh.1,000,000, Mipira 2,
Jezi Seti 1 na Cheti cha Ushiriki na mshindi wa tatu ataondoka na sh. 500,000,
Jezi Seti 1, na cheti cha Ushiriki wa ligi hiyo.
Katika
kuyafanya yawe na ushindani zaidi kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa Mchezaji
Bora wa mashindano, refa bora ambao wataondoka na sh. 100,000 kila mmoja huku
zawadi kwa kipa bora, kocha bora, timu yenye nidhamu na wanahabari bora wa
mashindano hayo wataondoka na sh. 50,000 kila mmoja.
Social Plugin