TUNDU LISSU AHUTUBIA MKUTANO MKUU CHADEMA TANZANIA AKIWA UBELGIJI


Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameuhutubia mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam akisema, mpango wa kukiua chama hicho iliyopangwa imeshindikana na zaidi imekiimarisha zaidi chama hicho.

Lissu amesema Madaktari wake wamemwambia amepona na yuko tayari kurudi Tanzania, kwa ajili ya kuungana na wanachama wenzake wa CHADEMA, na ameomba chama chake kimsaidie haraka iwezekanavyo aweze kurudi.

Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa jijini Dodoma na kupelekwa kutibiwa Nairobi nchini Kenya na baadaye nchini Ubelgiji, amedai kulikuwa na mpango wa kuua mfumo wa vyama vingi uliopangwa Februari 6 mwaka 2016.

“Yote yaliyotokea mpaka leo ni utekelezaji wa adhima hiyo ya kuua mfumo wa vyama vingi. Kwa ushahidi huu wa mkutano na mfumo wa uchaguzi katika chama mpaka siku ya leo, hicho walichokidhamiria hakijafanikiwa mpaka leo,” amesema Lissu leo Jumatano Desemba 18,2019

Akizungumza moja kwa moja akitumia ‘video call’ ya WhatApp kutoka Ubelgiji amesema, “baada ya mateso yote tuliyopata, baada ya bonde la uvuli wa mauti, njia iliyobaki ni kuchukua nchi mwaka ujao. Hakuna walichobakiza, watumefunga, wametujeruhi na kila mateso, leo tuna nguvu zaidi kuliko tulivyokuwa.”

Amewataka wana Chadema kufanya maandalizi ya kutosha ili ngwe iliyobaki aliyosema siyo ndefu na itakuwa ili wairudishe nchi katika utu, demokrasia na haki za binadamu.

Kuhusu afya yake, amesema madaktari wake wamesema amepona na yuko tayari kurudi nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post