Wadau wanaotetea haki za wanawake na watoto wametakiwa kutimiza wajibu wao ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa katika jamii.
Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 7,2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP), Christina Kamili wakati wa kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC).
Kikao hicho kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kikao hicho kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kamili ambaye ni Mwanasheria alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ni vyema kila mmoja akatimiza wajibu wake na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani wanaotenda ukatili wapo katika jamii.
“Kila mmoja akisimama bila kuwa na huruma,akasimamia sheria kama inavyotakiwa hizi tabia za ukatili dhidi ya wanawake na watoto zitakomeshwa.Hawa wanaofanya vitendo vya ukatili wapo katika jamii,wapo katika familia,kinachotakiwa ni kila mtu atimize wajibu wake”,alisema.
“Tunataka kuhakikisha ustawi wa mtoto na mwanamke unalindwa.Tunaomba pia utaratibu wa kuendesha kesi za jinai ufuatwe,tuache huruma kwenye kesi za jinai.Tukifanya mazoea hatumaliza kesi hizi.Kama kesi zimeharibiwa kuanzia mwanzo hata mwisho wa kesi pia utakuwa mbaya”,aliongeza Kamili.
Naye Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema changamoto iliyopo ni kwamba kamati zimeundwa lakini hazikutani kama mwongozo unavyoelekeza kwa madai kuwa hakuna pesa kwa ajili ya kuendesha shughuli za MTAKUWWA ngazi ya kata.
Katika hatua nyingine Ngangala alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake bado vinaendelea kujitokeza kwa sababu ya imani potofu iliyojengeka kwenye jamii.
"Tufichue uovu na asiyewajibika achukuliwe hatua ili kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii ikiwemo kuozesha watoto katika umri,kutumikisha watoto,kutopeleka watoto wa kike shule. Wengine wanabaka watoto ili wapate mali kutokana na imani za kishirikina. Vitendo hivi kavikubaliki",alisema Ngangala.
Kikao hicho kimehudhuriwa na maafisa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii watendaji wa kata,maafisa wa polisi kutoka dawati la jinsia na watoto,mahakimu wa mahakama za mwanzo,maafisa elimu na wadau wengine ikiwemo Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizunnguza katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizunnguza katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP),Christina Kamili akizungumza katika kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto kilicholenga kupata mrejesho kutoka kwenye jamii juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kupitia kamati zilizoundwa na TVMC katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP), Christina Kamili akiwasisitiza wadau wa haki za wanawake na watoto kutokuwa na huruma panapotokea vitendo viovu ikiwa ni pamoja kufuata taratibu za kuendesha kesi za jinai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP),Christina Kamili akizungumza katika kikao hicho.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Afisa Ustawi wa Jamii kata ya Didia, Felister Melli akitoa mrejesho kuhusu shughuli za utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata hiyo. Alisema changamoto iliyopo sasa ni wanaume wengi wanatelekeza familia zao.
Afisa Mtendaji kata ya Samuye, Melchades Oswald Kamuzora akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata yake. Alisema kesi za mimba kwa wanafunzi zimepungua katika kata hiyo.
Afisa Mtendaji kata ya Tinde, Latifa Mwendapole akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA katika kata yake.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akishauri namna ya kutekeleza shughuli za MTAKUWWA kikamilifu.
Afisa Elimu kata ya Masengwa,Juma Chiamba akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Samuye,Magai Magai akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Shinyanga ,Elizabeth Mweyo akichangia hoja katika kikao hicho.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akielezea namna ya kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, unaotekelezwa na Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT), Glory Mbia akichangia hoja katika kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Ilola,Bandi Sospeter ambaye pia ni Msaidizi wa Kisheria akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Mchungaji Dr. Meshack Kulwa akichangia hoja katika kikao hicho.
Kinaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin