Watanzania wametakiwa kutambua umuhimu wa kupima afya na kuchukua hatua za mapema ikiwa ni pamoja na kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI kwa kuwa waaminifu,kuzingatia matumizi sahihi ya Kondomu wakati wa tendo la ndoa.
Rai hiyo imetolewa leo Desemba 1,2019 na Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Nyabaganga Talaba wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack ,Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa UKIMWI upon a bado hauna chanjo wala tiba hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kupima afya zao na kuchukua hatua za mabadiliko ya tabia.
“Naomba tuachane na mila potofu zinazochochea maambukizi mapya ya VVU,wanaume jitokezeni kupata tohara na tuimarishe ulinzi wa watoto kwa kuwapa elimu ya madhara ya mahusiano ya mapema,mimba za utotni na kukemea mila kandamizi zinazochochea ndoa za utotoni ambazo ndiyo chanzo cha maambukizi ya VVU kwa watoto wetu”,amesema Nyabaganga.
Amesema mkoa wa Shinyanga unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya VVU yanapungua.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani mwaka 2019 ni ‘Jamii ni chachu ya mabadiliko tuungane kupunguza maambukizi mapya ya VVU’.
Miongoni mwa wadau waliofanikisha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani mkoani Shinyanga ni pamoja na Shirika lisilo la kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI ambalo linatekeleza kazi zake katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara.
Mashirika mengine yaliyoshiriki kwenye maadhimisho hayo ni CUAMM,Tanzania Redcross,JHPIEGO,Intrahealth International,THPS,Thubutu Africa Initiatives,USAID Tulonge Afya na DSW.
Nimekuwekea hapa picha za matukio yaliyojiri wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani mkoa wa Shinyanga Desemba 1,2019
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu leo Desemba 1,2019 - Picha zote na Kadama Malunde 1 blog.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Joachim Otaru akizungumza kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI mkoa wa Shinyanga,Dkt. Peter Mllacha akizungumza kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI mkoa wa Shinyanga,Dkt. Peter Mllacha akishikana mkono na viongozi mbalimbali baada ya kusoma taarifa ya UKIMWI mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Shirika la AGPAHI , Dkt. Nkingwa Mabelele akizungumza kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizungumza kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanajiri .
Shamra shamra zikiendelea wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Nyabaganga Talaba akicheza muziki na wadau mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Nyabaganga Talaba akisalimiana na wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani Kishapu wakati akielekea kukagua mabanda ya Mashirika mbalimba yaliyoshiriki kwenye Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu leo Desemba 1,2019
Hapa ni katika Banda la USAID Tulonge Afya : Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Nyabaganga Talaba akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mawasiliano Mabadiliko ya Tabia wa Mradi wa USAID Tulonge Afya mkoa wa Shinyanga, Mgalula Ginai jinsi wanavyotoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa mwananchi. Alisema pia wanaendelea kufanya uhamasishaji masuala ya upimaji wa VVU na matumizi sahihi ya dawa za kufubaza makali ya VVU kwa watu waliopata maambukizi ya VVU.
Kijana akitoa elimu ya matumizi sahihi ya Kondomu katika banda la USAID Tulonge Afya.
Hapa ni kwenye banda la Intrahealth International : Kulia ni Mtoa Huduma ya tohara ya hiari kutoka Intrahealth International,David Luhaga akitoa maelezo namna wanavyotoa huduma ya tohara kwa wanaume. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akisoma kipeperushi kuhusu Tohara kwa wanaume.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akielezea namna tohara kwa wanaume inavyopunguza hatari ya kupata maambukizi ya VVU.
Meneja wa Shirika la AGPAHI , Dkt. Nkingwa Mabelele akielezea shughuli zinazofanywa na shirika la AGPAHI katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akiangalia sabuni zinazotengenezwa na vijana wanaolelewa na shirika la AGPAHI.
Kulia ni Mratibu wa Upimaji VVU ngazi ya Jamii kutoka Shirika la Doctors with Africa - CUAMM, Dkt. Edith Kwezi akielezea kuhusu shughuli za shirika katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Meneja wa Upimaji VVU ngazi ya Jamii kutoka Shirika la Doctors with Africa - CUAMM, Veronica Censi akielezea mikakati mbalimbali waliyonayo kwenye mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Afisa Mradi wa Mlango ' Mlango Project' unaotekelezwa na shirika la Tanzania Health Promotion Support, Farida Myinga akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba namna wanavyoshiriki kupambana na kuzuia maambukizi ya VVU kwa makundi hatarishi.
Afisa Mradi wa Mlango ' Mlango Project' ,Farida Myinga unaotekelezwa na shirika la Tanzania Health Promotion Support akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba namna wanavyoshiriki kupambana na kuzuia maambukizi ya VVU kwa makundi hatarishi.
Kushoto ni Afisa Mradi wa Sauti wa shirika la JHPIEGO mkoa wa Shinyanga,Juma Jilala akielezea namna wanavyoshiriki katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na uchunguzi wa ukatili wa kijinsia.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akizungumza katika banda la JHPIEGO.
Msanii wa nyimbo za asili Jibhela Ngelela akiimba kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani.
Msanii Jibhela Ngelela akiendelea kutoa burudani.
Burudani ya sarakasi inaendelea.
Akina mama Ukenyenge wakiimba shairi
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Vijana wakiendelea kutoa burudani.
Vijana wakiendelea kutoa burudani kwa njia ya igizo.
Mwalimu Kassim Mwenda akihamasisha watu waliopata maambukizi ya VVU kuzingatia lishe na matumizi sahihi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.
Social Plugin