Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

URUSI NA UKRAINE ZAFIKIA MAKUBALIANO YA KUPITISHA GESI KUELEKEA ULAYA MAGHARIBI


Urusi na Ukraine zimesaini makubaliano ya upitishaji wa gesi ambayo yanaweza kuathiri eneo kubwa la Ulaya Magharibi.
 

Kampuni ya gesi inayomilikiwa na serikali ya Urusi, Gazprom, na ile ya nishati ya Ukraine, Naftogaz, zilifikia makubaliano jioni ya jana, baada ya wapatanishi kutumia siku kadhaa kupitia vipengele vya makubaliano hayo, kwa mujibu wa Rais Volo-dy-myr Zelensky wa Ukraine.

 Mkuu wa kampuni ya Gazprom ya Urusi, Alexej Miller, pia amethibitisha kufikiwa makubaliano hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi. 

Mkataba wa awali baina ya pande hizo mbili ulikuwa unamaliza muda wake leo baada ya kutumika kwa miaka kumi, ambapo mkataba huu mpya ni wa miaka mitano. 

Mataifa mengi ya Muungano wa Ulaya yanalitegemea bomba la gesi la Urusi linalopitia Ukraine. 

Hata hivyo, kwa miaka kadhaa mzozo baina ya nchi hizo mbili umekuwa ukiathiri makubaliano hayo ambayo yanaipatia Ukraine mabilioni ya euro.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com