Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amezindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji kwa wananchi wasajili laini zao za simu.
Uzinduzi huo ukiongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Haachwi mtu nyuma,kamilisha usajili’ umefanyika leo Jumatatu Desemba 2,2019 wakati wa Mkutano wa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole uliofanyika katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Akizungumza mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack amewataka wananchi kujitokeza kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole/kibaiometria ambao ni utaratibu wa kusajili laini za simu wa uhakika zaidi.
“Kitambulisho kinachoruhusiwa kutumika katika usajili wa laini za simu ni kitambulisho cha taifa kwani njia ya kibaiometria inafanyika kwa kutumia vifaa vya kielektroniki ambavyo vimeunganishwa kwenye mfumo wa vitambulisho vya taifa unaoratibiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)”,amesema Telack.
Amesema kutokana na changamoto ya wananchi kushindwa kusajili laini zao za simu kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha taifa,Telack amewaagiza maafisa wa NIDA mkoa wa Shinyanga kuweka kambi katika Uwanja wa Zimamoto kusaidia wananchi kupata namba za kitambulisho cha NIDA ili waweze kusajili laini za simu.
“Usajili wa laini unaendelea kufanyika kwenye maduka ya watoa huduma za mawasiliano na wakala wao na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 31,2019 ambapo laini ambazo hazijasajiliwa hazitaweza kutumika kwenye mawasiliano,NIDA ongezeni muda wa kuwa hapa ili muwasaidie wananchi wengi zaidi kupata namba za vitambulisho”,ameongeza Telack.
Mkuu huyo wa mkoa amewatahadhalisha wananchi kuachana na tabia ya kuazimana simu,kununua na kuuziana simu mtaani ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo pindi laini na simu kuonekana zimetumika kutekeleza vitendo vya uhalifu.
“Kila mtu anatakiwa asajili laini yake yeye mwenyewe,usithubutu kumsajilia mtu mwingine kwani endapo akifanya uhalifu vidole vilivyotumika kusajili vitaonekana ni vya kwako hivyo utajiingiza kwenye matatizo”,amesisitiza Telack.
Kwa upande wake, Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau amesema kati ya wananchi 619,915 waliojisajili NIDA,518,327 wameshapata namba za vitambulisho kwa ajili ya kutumia kusajili laini za simu.
Njau ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika kwenye ofisi za serikali za mitaa,vijiji na kata kwenda kuchukua namba za vitambulisho vya NIDA ili wasajili laini zao.
Akizungumza kwa niaba ya Makampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania, Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla amesema,makampuni ya simu yanaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuendesha zoezi la kuhamasisha wananchi wakamilishe usajili za laini zao za simu.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki amesema Usajili wa Laini za simu ni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (The Electronic and Postal Commucations Act) ya mwaka 2010 hivyo ni vyema kila mwananchi akasajili laini yake ya simu.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
kuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akionya wananchi kuacha tabia ya kuazimana simu,kununua na kuuziana simu mtaani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa kuzindua rasmi zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla
akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipiga picha na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipiga picha na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga leo Desemba 2,2019 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL namna wanavyoendesha zoezi la usajili wa laini za simu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL namna wanavyoendesha zoezi la usajili wa laini za simu.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisajili laini kwa kutumia kidole kwenye banda la Kampuni ya Simu ya TTCL.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akipokea laini ya TTCL baada ya kusajili kwa kutumia kidole kwenye banda la Kampuni ya Simu ya TTCL.
Kundi la sanaa ' Shinyanga Art Group' linaloongozwa na Msanii Chapchap likitoa burudani.
Afisa Msajili NIDA mkoa wa Shinyanga,Nathanael Njau akitoa maelekezo kwa wananchi namna ya kupata namba za kitambulisho cha NIDA kwa kutumia simu ya mkononi kwa kutuma ujumbe kwenda namba 15096 bure.
Afisa Msajili NIDA wilaya ya Shinyanga, Haruna Mushi akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliojitokeza kuchukua namba za vitambulisho vya NIDA kwenye Banda la NIDA.
Afisa Msajili NIDA wilaya ya Shinyanga, Haruna Mushi akiwasaidia wananchi kuchukua namba za vitambulisho vya taifa kwenye Banda la NIDA.
Wananchi wakiwa kwenye foleni kuchukua namba za vitambulisho vya taifa kwenye banda la NIDA.
Zoezi la Usajili likiendelea katika Banda la NIDA ambapo wananchi wengi wamejitokeza kujiandikisha/kujisajili ili wapate vitambulisho vya taifa.
Wafanyakazi wa Vodacom wakiuza simu za mkononi.
Zoezi la usajili wa laini likiendelea katika banda la Halotel.
Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ukiendelea katika banda la Vodacom.
Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ukiendelea katika mabanda ya Tigo
Burudani kutoka kundi la Shinyanga Art Group ikiendelea.
Ma DJ na ma MC mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Msanii Chapchap akitoa burudani ya wimbo.
Kaimu Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla akiagana na Afisa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kutoka TCRA, Walter Mariki baada ya kuzindua zoezi la Usajili wa Laini za simu kwa alama za vidole katika mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin