JESHI LA MAGEREZA LAONYA MATAPELI MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA



Pichani ni Gereza Kuu la Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Jeshi la Magereza nchini Tanzania, limetoa tahadhari kwa wananchi ambao ndugu zao bado wanatumikia vifungo magerezani, kujiepusha na matapeli wanaotumia mwanya wa msamaha wa Rais Magufuli kwenda kuwaomba pesa ili wawasaidie ndugu zao kuachiwa huru.

Kufuatia taarifa iliyotolewa leo Disemba 15, 2019, na msemaji wa Jeshi hilo Amina Kavirondo, imewataka wananchi kuacha kudanganywa na kwamba mtu anayestahili kutoa msamaha kwa wafungwa ni Rais wa Tanzania pekee.

"Mtu yeyote atakayejitokeza na kudai ana uwezo wa kusaidia ndugu aliyefungwa gerezani kunufaikwa na msamaha huo apuuzwe kwa kuwa hana mamlaka hayo na taarifa za tukio hilo zitolewe haraka kwenye vyombo vya Sheria" imeeleza taarifa ya Amina Kavirondo.

Disemba 9,2019, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania, ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 5,533, Nchi nzima.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post