Waziri wa Madini Doto Biteko, akizungumza na Wafanyabiashara ya Madini
katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mount Meru jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Doto Biteko, akiongea na Wafanyabiashara ya Madini
katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mount Meru jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko
Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo (kulia), na (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya
Madini Pro. Idris Kikula wakijadili jambo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Arusha.
Waziri wa Madini Doto Biteko watatu kutoka Kushoto, kutoka
kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Zelothe
Steven Zelothe na wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Madini wakiwa kwenye Soko la Madini jijini Arusha.
Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akiwa na Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
Na Tito Mselem,
Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wafanyabiashara wa
Madini ya Vito kote nchini kuhakikisha wanafanya biashara zao kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Serikali.
Waziri Biteko ameyasema hayo Desemba 21, 2019 wakati
akizungumza na Wafanyabiashara wa Madini (Dealers na Brokers) kwenye
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mount Meru, jijini Arusha.
Waziri Biteko amewatahadharisha wafanyabiashara wote
kwamba, wale wote wanaofanya vitendo vilivyo kinyume na taratibu
zilizowekwa na serikali watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amesisitiza suala la
Sheria na Kanuni zinazohusu masoko na uongezaji thamani wa madini ya
vito pamoja na masharti ya leseni wanazomiliki.
“Nipende kueleza kwamba, wale wote wanaofanya biashara ya
madini kwa kufuata Sheria na Taratibu hawatabuguziwa na mtu yoyote,
hivyo niwaombe wadau wote waa madini kufuata taratibu”, Waziri Biteko
alisema.
Wakati huo huo, Waziri Biteko, amevitaka vyama vyote vya
madini nchini kushirikiana na kupendana katika biashara ya madini na
kueleza, kwamba, kwenye biashara ya madini kuna majungu mengi ambayo
hayana tija.
Aidha, Waziri Biteko amevipongeza vyombo vya ulinzi na
usalama kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kusimamia na kulinda
rasilimali madini nchini.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli anawapenda sana wafanyabiashara na wachimbaji wa madini lakini
anachukizwa sana akisikia kwamba kuna mtu amekamatwa akitorosha madini
au anakwepa kodi ya serikali,” alisema Waziri Biteko.
Awali, Waziri Biteko alitembelea soko la Madini la jijini
Arusha na kuwapongeza wafanyabiashara wote wa madini kwa kufuata agizo
la serikali la kuhamishia shughuli za madini katika soko
hilo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Anthony
Mavunde, amesema Nchi inawahitaji wataalamu wa madini kwa asilimia kubwa
na kuanzia mwakani Wizara yake itaanza kuweka mikakati ya upatikanaji
wa vibali vya ajira kwa wageni kwa haraka.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amempongeza
Waziri wa Madini Doto Biteko, kwa usimamizi mzuri wa Rasilimali Madini
nchini na juhudi kubwa anazo zifanya katika kutatua changamoto
wanazozipitia wafanyabiashara na wachimbaji wa madini nchini.
“Nichukue fursa hii, kuwataka wadau wote wa madini nchini
kumuunga mkono Waziri wa Madini kwa kufuata Sheria naTaratibu
zilizowekwa na serikali na kuachana na suala la kutorosha madini,” Gambo
alisema.
Pia, Mwenyekititi wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula,
amesema Tume ya Madini imejipanga kikamilifu kuhakikisha leseni
zinatolewa kwa wakati kwa waombaji na kuimarisha usimamizi wa Masoko ya
Madini nchini.
Nae, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Madini,
Edwin Igenge ameeleza kwamba Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2017 inatoa mwongozo kwa shughuli zote za madini
nchini na kuwataka wadau wote wa madini kusoma Sheria mpya ya madini ili
waelewe miko na taratibu za shughuli hiyo.
Social Plugin