Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe ametoa pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wizara itaendelea kushirikiana na Bw.Karia ili kuhakikisha mafanikio ya CECAFA yanafikiwa katika kipindi cha uongozi wake pamoja na kuendeleza soka la hapa nchini.
Bw. Karia anachukua nafasi ya Mutasim Gaffar wa Sudan aliyemaliza muda wake na ataongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia sasa, huku akiwa Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo baada ya Bw.Leodger Tenga.
Aidha, nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais imechukuliwa na Francis Amin wa Sudan Kusini na nafasi ya Makamu wa Pili Rais imechukuliwa na Jira Isayaa kutoka Ethiopia. Imetolewa na,
Anitha Jonas
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Social Plugin